Sheria tata ya haki ya vijana ili wasilishwa na serikali ya Queensland, ndani ya bunge la jimbo mwisho wa Novemba.
Serikali ya shirikisho imetangaza ita waondoa waendeshaji wa mfumo waku kodi kwa ajili yaku nunua, kwa mfumo wayo wa malipo ya Centrepay, kama sehemu ya mageuzi mapana yenye lengo laku sitisha unyanyasaji wakifedha wa waAustralia wanao kabiliana na wakati mgumu.
Idadi ya wateja wa umeme wanao ingia katika miradi ya magumu ime ongezeka. Takwimu mpya kutoka Msimamizi wa nishati ya Australia [[AER]] kuanzia mwaka wa fedha wa 2023-24, hali inayo dokeza idadi ya wateja wanao ingia katika mipangilio ya magumu iliyo ongezeka kutoka asilimia 1.4 hadi asilimia 1.9.
Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza msamaha kwa mtoto wake Hunter, ambaye angehukumiwa mwezi huu kwa makosa ya kumiliki silaha na kodi na huenda angehukumiwa kifungo cha miaka kadhaa. Biden kwa miezi kadhaa aliahidi kutompa msamaha mtoto wake mwenye umri wa miaka 54, wakili ambaye kwa miaka kadhaa aligubikwa na tatizo la uraibu wa cocaine huku maisha yake yakididimia bila ya kudhibitiwa.
Mkutano mpya wa kilele wa kuendelea na mchakato wa amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo utafanyika Disemba 15 katika mji mkuu wa Angola, Luanda.
Mkutano huo utahudhuriwa na marais wa Rwanda Paul Kagame na Félix Tshisekedi wa Kongo.
Rais wa Kenya William Ruto amesema siku ya Jumamosi yeye na Rais wa Uganda Yoweri Museveni watasaidia kupatanisha Ethiopia na Somalia katika mzozo unaotishia kuvuruga ukanda wa Pembe ya Afrika. Ethiopia isiyo na bandari, ambayo ina maelfu ya wanajeshi nchini Somalia kupambana na waasi wenye mafungamano na al Qaeda, imeikasirisha serikali ya Mogadishu kwa mpango wake wa kujenga bandari katika eneo lililojitenga la Somaliland.