Wakaaji wana onywa wajiandae kwa uwezekano wa mafuriko “yanayo tishia maisha”, wakati kimbunga chaki tropiki Alfred kina karibia eneo la Kusini mashariki Queensland, pamoja na kaskazini New South Wales. Wakati huo huo kiongozi wa Queensland David Crisafulli, amesema wakaaji wanastahili “fanya wawezavyo” kuwa na vyakula vya mkebe, na vifaa vya dharura, kuweka vitambulisho vyao karibu pamoja naku ondoa taka katika mali zao.
Msanii wa Marekani Angie Stone, ame fariki akiwa na miaka 63. Mwakilishi wa muimbaji huyo amethibitisha kuwa, alifia katika ajali ya gari mjini Montgomery, Alabama. Imeripotiwa, alikuwa njiani akirejea nyumbani kutoka tamasha, na ni yeye pekee aliyefariki katika ajali hiyo.
Uingereza, Ufaransa na Ukraine zimekubaliana kufanyia kazi mpango wa kusitisha mapigano kuwasilishwa kwa Marekani, Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, amesema Jumapili alipokuwa akijiandaa kuwa mwenyeji wa mkutano wa viongozi wa Ulaya kujadili kumaliza vita. Mkutano huo umegubikwa na kuzomewa vikali kwa rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, na Rais wa Marekani, Donald Trump, kwa “kutoshukuru uungwaji mkono wa Marekani” katika vita vya Ukraine dhidi ya uvamizi wa Russia, wakati walipokutana Ijumaa katika White House.
Wasiwasi wa kutanuka vita vya Mashariki mwa DRC,kuwa vya kikanda,waongezeka. Jeshi la Uganda limethibitisha kutuma kikosi chake katika mji mwingine kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kukabiliana na makundi ya waasi kwenye eneo hilo. Hatua ya Uganda imekuja chini ya kiwingu cha wasiwasi kwamba vita vya Mashariki mwa Kongo huenda vikatanuka na kuwa vita kamili vya kikanda.
Katika mchezo wa kriket, Australia ita kabiliana na India katika nusu fainali ya kwanza ya kombe la mabingwa mjini Dubai Jumanne 4 Machi. Ushindi wa India wa mikimbio 44 dhidi ya New Zealand katika uwanja wakimataifa wa Dubai, ume ipa fursa yaku menyana na Australia katika nusu fainali hiyo.
Cooper Connolly atachukua nafasi ya Matthew Short ambaye amejeruhiwa katika kikosi cha Australia.