Taarifa ya Habari 4 Disemba 2023

City - Swahili.jpg

Kiongozi wa upinzani Peter Dutton amelaani anacho elezea kuwa ongezeko la mashambulizi dhidi ya wayahudi nchini Australia, tangu mwanzo wa mapigano mapya kati ya Israel na Hamas.


Akizungumza katika mkutano wa viongozi wakidini wa wayahudi jimboni  New South Wales ndani ya hekalu moja mjini Sydney, Bw Dutton amesema Australia inapitia uzoefu wa mashambulizi dhidi ya wayahudi kwa kiwango ambacho hakija wahi onekana. Amewakosoa wale ambao ame elezea kuwa wana panda migogoro yakijamii katika demokrasia yetu na, ameomba serikali iitishe kuachiwa huru kwa mateka wote wa Israel, kwa kutumia vifaa vyote vyakidiplomasia.

Waziri wa kilimo wa shirikisho Murray Watt ametoa onyo kali kwa masoko zisijaribu kupata faida kupitia wa Australia wanao fanya kazi kwa bidii tunapo elekea katika krismasi.

Wito wake umejiri wakati soko kama Coles na Woolworths zinatarajiwa kufika mbele ya kamati ya bunge kujibu maswali kama wana ongeza bei ya bidhaa zao zaidi wakati wateja wanakabiliana na shinikizo za gharama ya maisha. Kamati hiyo iliyo itakayo anzishwa wiki hii, itaongozwa na chama cha Greens ita chunguza bei za vyakula, mamlaka ya soko pamoja na faida kubwa wakati mabosi soko zote mbili kubwa wakitarajiwa kuitwa katika vikao hivyo.

Wafungwa wa uhamiaji hivi karibuni wata wekwa chini ya masharti ya vifungo sawia na wahalifu wenye hatari ya kiwango cha juu wa ugaidi. Serikali ya shirikisho inatarajiwa kuwasilisha mageuzi wiki hii kwa sheria zilizo letwa, kukabiliana na utata ulio ibuka baada ya hukumu ya mahakama kuu, iliyo amuru kuwa kufungwa kwa muda usiojulikana si halali. Hukumu hiyo ilisababisha zaidi ya wafungwa 140 kuachiwa huru. Chini ya mageuzi hayo, amri zakuwekwa kizuizini zita tumiwa kwa walio achiwa huru, kundi hilo likiwajumuisha wauaji, na wahalifu wa ngono. Hatua hiyo ikiwa sambamba na wahalifu wenye hatari ya juu wa ugaidi.

Watu wasiopungua 47 wamefariki na 85 wengine wamejeruhiwa kutokana na mafuriko katika mkoa wa Manyara huko kaskazini mwa Tanzania kutokana na mvua kubwa iliyosababishwa na hali ya hewa ya El Nino. Mkuu wa mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amesema mpaka majira ya saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki siku ya Jumapili vifo vilifikia idadi hiyo ambapo pia kulikuwa na uharibifu wa mali za watu wilayani humo.
Wakati huo huo Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa mjini Dubai akihudhuria mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa COP28, alitoa salamu za rambirambi kwa njia ya video akiwapa pole wale walioathiriwa na maafa hayo katika kipindi hiki cha mvua za El Nino zinazoendelea kunyesha katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki. Mvua hiyo ilisababisha sehemu ya mlima Hanang kumomonyoka na kusababisha tope kubwa kutiririka katika maeneo ya Katesh na Gendabi.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limeitaka serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuchukuwa hatua dhidi ya matukio yanayosababishwa na chuki baada ya mwanajeshi wa Kitutsi kuuawa. Shirika hilo la kutetea haki za binadamu limesema Luteni Patrick Gisore Kabongo aliuawa katika mji wa mashariki wa Goma mnamo Novemba 9 katika tukio linalodhaniwa kuwa lilichochewa na chuki za kikabila.   Mwanajeshi huyo, aliyekuwa na umri wa miaka 42 na aliyekuwa wa kabila la Tutsi kutoka Kivu Kusini, alishutumiwa na waasi wa M23 kwamba tabia zake zilikuwa tofauti na wao, kulingana na Human Rights Watch.

Katika michezo mji wa Gold Coast umefuta ombi lake lenye thamani $700 milioni kuwa mwenyeji wa michezo ya jumuiya yamadola ya 2026, baada ya mji huo kufeli kuungwa mkono kutoka kwa serikali za jimbo na shirikisho.

Halmashauri hiyo ya jiji ambalo liko Queensland, ilikuwa imependekeza mfumo sawia na ule wa serikali ya Victoria iliyo jiondoa Julai kwa sababu ongezeko ya gharama ya maandalizi. Katika taarifa, meya wa mji wa Gold Coast Tom Tate alisema mji wa wake ulijaribu uwezavyo ila, sifa ya Australia kama sehemu inayo kiuka mikataba ya michezo yakimataifa, inaendelea kuharibika.


Share