Bunge la shirikisho lime rejea leo kwa vikao vya wiki mbili, katika vikao ambavyo vinaweza kuwa vya mwisho kabla ya uchaguzi mkuu kutangazwa.
Dharura ya mafuriko yampeleka waziri wa Huduma za Dhurua Kaskazini Queensland, wakati moto wa vichaka waendelea kukabiliwa jimboni Victoria na Tathmini ya sheria za usalama wa mtandaoni imependekeza faini kubwa kwa makampuni ya mitandao yakijamii, ziki feli kuwalinda wa Australia dhidi ya madhara ya mtandaoni.
Kauli hiyo inafuatia miito ya ndani ya nchi yake ya kutaka wanajeshi wa Afrika ya Kusini walioko Kongo warejeshwe nyumbani baada ya kuuliwa kwa wanajeshi 14 huko Kivu Kaskazini. Kuuliwa kwa wanajeshi 14 wa Afrika ya Kusini huko Sake na Goma, jimboni Kivu Kaskazini kumeibua mjadala mkali nchini humo.
Maafisa wa Uganda wanajiandaa kupeleka chanjo ya majaribio kama sehemu ya juhudi za kukomesha mlipuko wa Ebola katika mji mkuu, Kampala, afisa mkuu wa afya amesema siku ya Jumapili.
Muungano wa mashirika ya kijamii umesisitiza kuwa uainishaji wa mipaka unaweza kufanywa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027. Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ilifaa kuratibu upya mipaka ya ndani ya nchi kufikia Machi 2024 lakini hakukuwezekana kwa sababu ya kukosa tume kamili baada ya muhula wa baadhi ya makamishna kupita, wengine kujiuzulu ama kutimuliwa.