Waziri Gallagher ameongezea kuwa serikali imekuwa ikifanya kazi kupunguza nakisi zozote katika bajeti, yakiwemo mageuzi kwa mfumo wa NDIS na malezi ya uzeeni ambayo, yata ondoa shinikizo kwa bejeti katika muda wa kati.
Serikali ya shirikisho imetangaza uwekezaji wa dola bilioni 4.8 katika shule za New South Wales, uwekezaji huo uta anza kutumiwa mwakani iwapo chama cha Labor kita shinda uchaguzi mkuu. Chini ya makubaliano hayo, kwa zaidi ya miaka 10, uwekezaji huo utawafikia wanafunzi 780,000 na, kuinua mchango wa serikali ya madola kwa mfumo mkubwa zaidi wa shule ya Australia, kwa asilimia 5 nakufukisha uwekezaji huo kuwa asilimia 25. Majimbo yote na wilaya isipokuwa Queensland kwa sasa zimefikia makubaliano na serikali ya shirikisho kwa jeki ya uwekezaji wa elimu ya umma chini ya kile ambacho serikali ya shirikisho ime ita, makubaliano bora na ya usawa wa shule.
Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limekanusha juu ya kukamatwa kwa wapiganaji 20 wa kundi la FDLR wanaohusishwa na mauaji ya kimbari ya Rwanda kwenye ardhi yake, na kulishutumu kwa uhalifu wa kivita. Kundi la waasi la M23 mwishoni mwa juma lilitoa taarifa ya kuwakamata wapiganaji wa kundi la wanamgambo wa kihutu la FDLR. waliohusika katika mauaji ya Watutsi nchini Rwanda mnamno mwaka 1994. Taarifa ya jeshi la Kongo imesema tukio hilo ni la kubuni na lilikuwa na lengo la kulidhihaki jeshi la Kongo na kuongeza kwamba kusambaa kwa video hiyo ni sehemu ya mkakati wa Rwanda kuhalalisha kile walichokiita uvamizi katika maeneo ya kimkakati nchini humo.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, ametetea msimamo mkali wa chama hicho kuhusu kauli mbiu ya “Hakuna Mageuzi, Hakuna Uchaguzi” na kusisitiza kuwa umejikita katika hitaji la mfumo wa uchaguzi. Katikati mwa mwezi Februari Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzani Tanzania, Chadema, Tundu Lissu alisema chama hicho hakitasusia uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu na badala yake kinakwenda kuhakikisha uchaguzi huo hautafanyika kabisa. Lissu aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa chama hicho Januari 22 amesema mifumo ya uchaguzi Tanzania inadhibitiwa na Rais wa nchi na kwa upande wa Zanzibar pia ukidhibitiwa na Rais.
Wizara ya afya nchini Kenya imesema ipo mbioni kupambana na mlipuko wa ugonjwa usiojulikana na ambao umeathiri zaidi ya watu 200 katika vijiji vitatu vya jimbo la Kisii eneo la Nyanza Magharibi ya Kenya. Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya anayehusika na afya ya umma Mary Muthoni anasema tayari maafisa wa serikali kwa ushirikiano na serikali ya jimbo la Kisii tayari wamefika maeneo yaliyoathiriwa kuchukua sampuli za vipimo zitakazofanyiwa uchunguzi chanzo cha maradhi hayo.