Taarifa ya Habari 6 Disemba 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Kura mpya ya maoni inadokeza kiongozi wa upinzani Peter Dutton, ana elekea kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu ujao.


Matokeo ya utafiti ya Accent Group na Redbridge Group walio shirikisha watu 5000 katika utafiti wao, yame tabiri upinzani wa mseto, kwa sasa una tarajiwa kushinda viti 42 na mseto huo uko mbele katika maeneo bunge mengine 22, wakati serikali ya Labor inatarajiwa kushinda viti 47 na iko mbele katika maeneo bunge mengine 12. Maeneo bunge yanayo tarajiwa kubalisha uongozi yanajumuisha maeneo bunge tano jimboni New South Wales.

Chama cha Madaktari cha Australia kimesema mfumo wa huduma ya afya ya akili, unafeli baadhi ya watu walio katika hali mbaya zaidi ndani ya jumuiya. Chama hicho kina omba serikali zote zifanye kazi pamoja kuwekeza katika afya ya akili, na kushughulikia uhaba mkubwa katika nguvu kazi.

Shirika linalo fanya harakati dhidi ya unyanyasaji wakijinsia, limezindua kampeni yake ya kwanza yakutoa uelewa kwa jina la 'Red Flag Day', kwa ajili yakutoa uelewa kwa dalili zinazo onesha mahusiano ya unyanyasaji. Shirika linalo fanya harakati dhidi ya unyanyasaji wakijinsia, limezindua kampeni yake ya kwanza yakutoa uelewa kwa jina la 'Red Flag Day', kwa ajili yakutoa uelewa kwa dalili zinazo onesha mahusiano ya unyanyasaji. Hali hiyo imejiri wakati wanawake 72 nchini Australia, wame uawa kwa sababu ya ukatili wa nyumbani na familia mwaka huu, ambayo ni sawia na mwanamke mmoja kila siku nne hadi tano.

Miji ya Perth, Adelaide na Brisbane imetabiriwa itapitia uzoefu wa ongezeko kubwa ya bei ya nyumba katika mwaka wa 2025, pakiwa uhaba sugu wa nyumba na makato ya viwango vya riba ikitarajiwa kufanya upatikanaji kuwa mbaya zaidi. Shirika linalo onesha nyumba mtandaoni Domain, katika muhtasri wao mwisho wa mwaka, lime tabiri kuwa shinikizo kwa wanunuaji linalo endelea, pamoja na mahitaji ya nyumba yata endelea kuongeza bei za nyumba. Nicola Powell ni afisa mkuu wa utafiti na uchumi katika kampuni ya Domain, amesema miji ya Sydney na Melbourne, inatarajia kupitia uzoefu wa ukuaji wa bei ndogo, wakati wanunuaji wana elekea katika miji midogo ambako thamani ziko chini.

Baada ya miezi minne, pamoja na kufukuzwa kwa ujumbe wa serikali, mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini yaliyokwama yameanza tena Jumatano nchini Kenya, ikiwa juhudi ya karibuni zaidi ya kumaliza ghasia ambazo zimevuruga kabisa uchumi na uthabiti wa taifa hilo changa.

Nchini Burundi, afisa mkuu wa serikali mapema wiki hii alipokuwa kwenye misheni ya kikazi nchini Ubelgiji, alimua kubaki nchini humo. Tukio hili lililojiri siku ya Jumatatu Desemba 2, 2024 wakati barua ya waziri wa Elimu iliyomteua mtu mwingine kushika nafasi yake ilionekana kwenye mitandao ya kijamii, na tangu wakati huo barua hii imezua gumzo. Lakini jambo hili ambalo huleta furaha kwa watumiaji wa Intaneti wa Burundi inaonekana kuwa jambo linalokasirisha utawala.

Ugonjwa wa kutatanisha umewauwa watu 143 katika mkoa wa kusini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, viongozi wa eneo hilo wameliambia shirika la habari la REUTERS. Idadi iliyothibitishwa kwa mwandishi wa BBC wa eneo hilo na Makamu wa Gavana wa mkoa huo na Waziri wa Afya wa mkoa. Hata hivyo, serikali ilisema katika taarifa kwa vyombo vya habari mnamo Desemba 4 kwamba ugonjwa huu umesababisha vifo vya watu 79.

Aliyekuwa waziri mkuu nchini Kenya, Raila Odinga atakabiliana na wapinzani wake katika wadhifa wa uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC) katika mdahalo wa televisheni utakaofanyika Desemba 13 kuwasilisha maono na mawazo yao ya kutekeleza Ajenda Afrika 2063. Mjadala Afrika, ni mdahalo wa moja kwa moja unaotoa jukwaa kwa wagombea kuhutubia raia wa Afrika, kwa kuzingatia masuala ya sera na mwelekeo kuhusu jinsi kila mgombea ananuia kuendeleza matarajio na malengo ya Ajenda 2063.
Wakati wa mdahalo huo, Raila atachuana vikali na wagombea wengine wawili; Mahmoud Ali Youssouf (Djibouti), Richard Randriamandrato (Madagascar).

Share