Taarifa ya Habari 6 Machi 2025

Bench - Swahili.jpg

Ofisi ya utabiri wa hali ya hewa, ime toa taarifa mpya kuhusu wakati kimbunga chaki tropiki Alfred, kina tarajiwa kufika katika nchi kavu.


Badala ya Usiku wa Alhamisi 7 Machi, ofisi hiyo imesema utabiri mpya unadokeza kuwa kimbunga hicho kitavuka pwani ya Queensland kati ya Maroochydore na Coolangatta jioni ya Ijumaa mida ya saa mbili za usiku. Idadi ya wakaazi milioni nne unusu pamoja na nyumba milioni 1.8, ziko katika maeneo yanayo tarajiwa kuathiriwa; kuanzia eneo la Double Island Point jimboni Queensland hadi Grafton jimboni New South Wales. Maeneo mengine yanayo tabiriwa kuathirika ni pamoja na Brisbane, Gold Coast, Sunshine Coast, Byron Bay na Ballina. Shule zimefungwa katika maeneo husika ya majimbo yote mbili, ikiwa ni zaidi ya shule 660 katika eneo la kusini mashariki Queensland, na zaidi ya shule 280 katika maeneo ya kaskazini New South Wales.

Mweka hazina wa shirikisho Jim Chalmers amesema Marekani bado haija fanya uamuzi kuhusu Australia kusamehewa kulipa ushuru. Rais wa Marekani Donald Trump alikuwa amesema atazingatia ombi la Australia kusamehewa kulipa ushuru wa asilimia 25, kwa mauzo yote ya vyuma nchini mwake. Bw Chalmers ame eleza shirika la habari la ABC kuwa, serikali imekuwa ikiwasiliana katika viwango vyote, kutetea kesi yake na majadiliano yana endelea.

Wanajeshi wa Sudan kusini wamezingira makao ya makam rais Riek Machar katika mji mkuu wa Juba. Washirika wa karibu kadhaa wa Machar wamekamatwa. Machar, ambaye uhasama wake wa kisiasa na rais Salva Kiir umepelekea vita vya wenyewe kwa wenyewe, alisema mwezi uliopita kwamba hatua ya rais Kiir kufuta kazi washirika wake wa karibu kutoka serikalini, inatishia makubaliano ya amani yam waka 2018 kati yake na Kiir, yaliyomaliza viya vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 5, vilivyosababisha vifo vya zaidi ya watu 400,000. Naibu wa mkuu wa jeshi la Sudan kusini Generali Gabriel Duop Lam, ambaye pia ni mshirika wa Machar, alikamatwa na kuzuiliwa Jumanne, akihusishwa na mapigano ya kaskazini.

Kisiwa cha Idjwi nchini Kongo ni eneo lililosahaulika ambalo limeishi kwa miongo kadhaa ya vita bila kuathirika. Kisiwa cha pili kwa ukubwa kilichoko ziwani barani Afrika, Idjwi, kipo katika sehemu ya kusini ya Ziwa Kivu, kikizungukwa na nchi mbili ambazo zimekuwa katika vita kwa karibu miongo mitatu: DRC na Rwanda. "Hatuna wanajeshi hapa, kutoka upande wowote. Hatujawahi kusikia milio ya bunduki au mabomu, lakini tunahisi athari za vita," anasema Yves Minani, mjasiriamali na mkurugenzi wa kituo cha redio cha ndani. Maisha katika kisiwa cha Idjwi yanaelezwa kuwa ya amani, na mazuri. Ni tofauti kabisa na sehemu za bara ambako waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wameteka miji miwili mikuu ya mkoa, Goma na Bukavu.

Katika michezo:

Kundi la wachazaje 35 wa kike jimboni Victoria walio jiondoa kutoka timu ya wanawake ya mchezo wa pete kwa jina la Kyneton Football Netball Club, kwa sababu ya wasiwasi kuhusu  usawa wakijinsia na unyanyasaji, wamesema hawana sehemu yakuchezea. Natalie Korinfsky ni rais wa timu mpya iliyo undwa kwa jina la Kyneton Women's Eagles football Club, timu hiyo iliundwa na wachezaji walio jiondoa katika timu yao ya zamani. Bi Korinfsky amesema tangu walipo ondoka kuanza timu ya huru, hawa wezi tumia tena vifaa vya timu yao ya zamani na hawaja pata ligi yakujiunga kucheza. Licha ya shutma hizo, timu yao ya zamani imesisitiza kuwa daima, imekuwa jumuishi iwezekanavyo.

Katika soka msanii wa kundi la Coldplay Chris Martin, atasaidia shirikisho la soka duniani FIFA kukamilisha orodha ya wasanii watakao fanya tamasha wakati wa mapumziko kwa mara ya kwanza katika mechi za soka wakati wa fainali ya kombe la dunia mwakani 2026. Tamasha hiyo imeratibiwa kufanywa katika uwanja wa MetLife Stadium mjini New Jersey. Rais wa FIFA Gianni Infantino alitoa taarifa hiyo katika tangazo lililo chapishwa katika mtandao wakijamii.

Share