Taarifa ya Habari 7 Februari 2025

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Serikali ya Wilaya ya Kaskazini ime fikia makubaliano ya thamani yama milioni ya dola na mashirika yawa Australia wa kwanza, kutoa huduma kwa maeneo ya vijijini.


Uwekezaji wa $842.6 milioni kwa Northern Territory Remote Aboriginal Investment utasimamiwa na serikali ya shirikisho kwa muda wa miaka sita, kwa huduma kama utoaji wa huduma za polisi, usalama wa wanawake, elimu, pamoja na kupunguza madhara ya vilevi, na kupiga jeki huduma zawa kalimani nakuendelea kuwekeza huduma za afya yaku sikia na afya ya kinywa.

Kwa mara nyingine maswali yana ulizwa kuhusu mazingira ya barabara kuu ya Bruce, kwa matukio makubwa ya hali ya hewa katika jimbo la Kaskazini Queensland. Baadhi ya jumuiya zime achwa zikiwa zime tengwa kwa sababu ya mafuriko yaliyo kata sehemu za barabara kuu katika sehemu, nakulazimisha mamlaka kupeleka baadhi ya vifaa muhimu kwa ndege kwa wakaaji.

Viongozi wa vyama vya wafanyakazi wanaomba pawe kodi ya watalii kwa miji ya kanda inayo kabiliana na wakati mgumu kupata, wafanyakazi muhimu kwa sababu ya gharama kubwa ya makazi.

Karibu watu 70 wameuwawa na wengine 50 kujeruhiwa kufuatia mapigano ya saa 24 kati ya wapiganaji wa Islamic State na vikosi vya eneo la Somalia la Puntland. Taarifa hizo zimetolewa na maafisa kadhaa wa usalama wa Puntland wakizungumza na vyombo vya habari kwa masharti ya kutotambulishwa kwa kuwa hawajaruhusiwa kuongea na vyombo vya habari.

Waasi wa M23 wametangaza nia yao ya “kuikomboa Kongo yote” wakati wa mkutano wa hadhara mjini Goma. Huku kundi hilo likisonga mbele kuelekea mji mkuu mwingine wa mkoa, hofu ya machafuko zaidi inazidi kuongezeka. Akihutubia maelfu ya watu katika uwanja wa michezo uliojaa Goma, Corneille Nangaa, mkuu wa muungano wa kisiasa na kijeshi unaojumuisha M23, aliomba dakika moja ya ukimya kwa wahanga wa mapigano kabla ya kuapa kumuondoa madarakani Rais wa DRC, Felix Tshisekedi.

Mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye, ataendelea kusalia kizuizini licha ya uamuzi wa wiki iliyopita wa mahakama ya juu, ambayo ilitamka kuwa kinyume cha sheria kwa mahakama ya kijeshi kusikiliza kesi za raia wa kawaidia. Mawakili wa Dkt Besigye na Hajji Lutale wakiongozwa na Martha Karua wame kuwa wakishinikiza kuachiliwa kwao bila mafanikio.

Share