Taarifa ya Habari 7 Machi 2025

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Waziri Mkuu Anthony Albanese amesema ame idhinisha ombi la wanajeshi 120, watakao enda mara moja New South Wales kusaidia katika juhudi zaku kabiliana na Kimbunga Alfred.


Utabiri mpya kutoka ofisi ya utabiri wa hali ya hewa, ume rudisha nyuma wakati ambapo kimbunga Alfred kinatarajiwa kufika katika nchi kavu hadi asubuhi ya Jumamosi mida ya saa tano asubuhi kwa masaa ya Mashariki ya Australia. Takriban wakaaji milioni 4.5 na takriban nyumba milioni 1.8 ziko katika eneo ya hatari.

Kabla ya uchaguzi wa shirikisho ujao baadae mwaka huu, ushiriki wa wapiga kura una endelea kuzua wasiwasi katika wilaya ya kaskazini, wakati baadhi ya jumuiya zawa Australia wa kwanza wana endelea kutengwa kwa sababu ya hali mbaya ya hewa. Tume ya uchaguzi ya Australia (AEC) imethibitisha kuwa timu 24 zita tembelea jumuiya 200 katika wilaya ya kaskazini, kwa kutumia ndege zilizo kodishwa na hata helikopta, kuwafikia wapiga kura vijijini. Jimbo la Magharibi Australia na Wilaya ya Kaskazini zina viwango vya chini vya usajili vya wa Australia wa kwanza ambavyo katika jimbo la Magharibi Australia ni asilimia 86.1 wakati katika Wilaya ya Kaskazini kiwango cha usajili ni 87.9

Tathmini ya dhamana ambayo imesubiriwa kwa muda mrefu ya jimbo la Victoria ime harakishwa, wakati takwimu za uhalifu zina onesha uvamizi wa nyumba ambako wakaazi wako ndani au mhalifu alikuwa na silaha, imeongezeka mara mbili jimboni humo katika mungo uliopita. Mwanasheria mkuu sasa amesema tathmini hiyo ita tolewa hivi karibuni. Katika miezi 12 hadi Septemba 2015, kulikuwa kesi 2576 za uvamizi wa makaazi binafsi, kulinganisha na kesi 6390 katika mwaka hadi Septemba 2024.

Wanajeshi wa Sudan kusini wamezingira makao ya makam rais Riek Machar katika mji mkuu wa Juba. Washirika wa karibu kadhaa wa Machar wamekamatwa. Machar, ambaye uhasama wake wa kisiasa na rais Salva Kiir umepelekea vita vya wenyewe kwa wenyewe, alisema mwezi uliopita kwamba hatua ya rais Kiir kufuta kazi washirika wake wa karibu kutoka serikalini, inatishia makubaliano ya amani yam waka 2018 kati yake na Kiir, yaliyomaliza viya vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 5, vilivyosababisha vifo vya zaidi ya watu 400,000.

Jeshi la Kongo linamtuhumu mbabe wa zamani wa kivita Thomas Lubanga Dylo kwa kuunda kundi jipya lenye silaha liitwalo Convention for Popular Liberation (CRP). Kwa mujibu wa msemaji wa FARDC kundi hilo jipya la waasi huko Bunia na lenye makazi yake nchini Uganda, linashirikiana na waasi wa M23 kulivuruga jimbo la Ituri.

Afrika Kusini imesema Marekani imejiondowa kwenye mpango wa kufadhili miradi ya kutunza mazingira, uliofikiwa kati ya mataifa tajiri kuyasaidia mataifa washirika wao yanayoendelea. Afrika Kusini ndio nchi ya kwanza kufaidika na mpango huo. Mpango huo unaofahamika kama JETP, unahusisha kundi dogo la mataifa tajiri na mataifa yanayoinukia kiuchumi kuyasaidia kuondokana na matumizi ya makaa ya mawe.

Share