Taarifa ya Habari 8 Disemba 2023

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili.jpg

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Majimbo kadhaa yame wekwa katika tahadhari ya juu ya moto wa vichaka, mazingira ya joto kali yakitabiriwa wikendi hii.


Shirika la Country Fire Service limeonya leo disemba 8, inaweza kuwa moja ya siku muhimu zaidi kwa hali ya hewa ya moto, onyo kali au maafa yametabiriwa katika sehemu nyingi za New South Wales, sehemu za Kusini Australia na Victoria.

Nyuzi joto katika jimbo zima la Kusini Australia zinatarajiwa kufika kati ya 40 leo, wakati mazingira ya joto yanatarajiwa kuendelea kwa siku kadhaa katika jimbo la N-S-W, miale ya umeme wa radi ikiongeza hatari ya moto.

Waathirika wa unyanyasaji wa nyumbani wataweza pata ushauri kutoka kwa wataalam pamoja na msaada kwa ujumbe mfupi wa simu chini ya mpango mpya ulio undwa kufanya kutafuta msaada kupatikana zaidi. Waziri wa huduma za jamii Amanda Rishworth hii leo amezindua mfumo huo ambao chini ya msaada kwa ujumbe mfupi wa simu kwa namba ya unyanyasaji wakijinsia ambayo ni 1800RESPECT, itapatikana kwa masaa 24 ya siku, siku saba za wiki sambamba na simu na huduma za mtandaoni.

Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amewataka wabunge wa chama chake cha Conservative siku ya Alhamisi kuunga mkono mpango wake wa kuwapeleka Rwanda waomba hifadhi baada ya mpango huo kukataliwa na kubainisha migawanyiko mikubwa ndani ya chama chake.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu amesema serikali imepata maeneo ya kuwahamishia waathirika wa janga la mafuriko na maporomko ya udongo wilayani Hanang kaskazini mwa nchi hiyo na itahakikisha hilo linafanyika kwa haraka. ''Wataalamu wamepata eneo la kuwahamishia, serikali itahakikisha inashirikiana nao ili kufanya hilo kwa haraka''. amesema Rais Samia.

Kenya inawapeleka wafanyakazi 1,500 wa mashambani nchini Israel, wizara ya kazi imesema. Tangazo hilo linakuja takriban wiki mbili baada ya Malawi kuwapeleka vijana 221 kufanya kazi katika mashamba ya Israel, na kusababisha lawama dhidi ya serikali. Wafanyakazi hao wa kawaida watatumwa kwa kandarasi za miaka mitatu inayoweza kuongezwa, "na mapato ya uhakika" ya $1,500 (£1,195), wizara ya kazi iliongeza.

Zikiwa zimesalia takribani wiki mbili raia wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wapige kura kumchagua Rais atakayeiongoza nchi hiyo, wagombea wa urais wanaendelea kunadi sera zao katika maeneo tofauti nchini humo. Rais wa nchi hiyo Felix Tshisekedi atanadi sera zake jimboni Tanganyika ikiwa ni mara ya kwanza kuingia jimboni humo tangu alipochaguliwe kuwa kiongozi wa nchi hiyo.


Share