Taarifa ya Habari 8 Juni 2021

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Serikali ya Magharibi Australia yawaruhusu, watu wenye kati ya miaka 30 hadi 49, kupokea chanjo ya coronavirus kuanzia Alhamisi na mamlaka wa afya wa Victoria, wazingatia kuregeza vizuizi jimboni humo.


Chama cha shirikisho cha Labor, kimeongeza wito kwa serikali ya taifa iwape uhamisho familia yawaomba hifadhi yaki tamil ambayo imefungwa ndani ya Christmas Island. Familia hiyo imekuwa katika kisiwa hicho tangu Agosti 2019 wakati, uamuzi wa mahakama ulizuia familia hiyo kurejeshwa Sri Lanka.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ametangaza kutogombea uenyekiti wa chama hicho kwenye uchaguzi wa mwaka 2023 ingawa tangazo hilo lililotolewa pasi na mbwembwe za namna yoyote, licha ya kuwa mwangwi wake ni mkubwa katika siasa za Tanzania.

Rais wa Marekani Joe Biden amesema nchi yake itasimama imara na washirika wake wa Ulaya dhidi ya Russia, kuelekea kwa mkutano wa kwanza wa ana kwa ana na rais Vladimir Putin.

 


Share