Katika hotuba yake waziri mkuu, ali waeleza wabunge kuwa demokrasia ni mfumo bora waku tatua matatizo na, kuheshimu matokeo katika demokrasia ni muhimu pia.
Serikali ya Magharibi Australia imetangaza mfango mpya wakununua bunduki, kabla ya sheria mpya za silaha kuanza kutumika jimboni humo. Wauzaji wenye silaha wenye leseni ya serikali wanaweza salimisha bunduki zao kwa jeshi la polisi la WA, nakupewa $1,000 kutegemea na hali ya silaha hiyo. Mpango huo uta tumika hadi mwakani, nakuweka kikomo kwa idadi ya bunduki mtu mmoja anaweza miliki.
Upinzani wa mseto umekaribisha mpango wa serikali wakupiga marufuku watoto wenye chini ya miaka 16, kutumia mitandao yakijamii. Waziri Mkuu Anthony Albanese jana Alhamis 7 Nov alitangaza anapanga kuwasilisha muswada wa marufuku mwaka huu, ambao uta anza kutumiwa miezi 12 baada ya muswada huo kupitishwa na uta husu watumiaji wa mtandao wakijamii wa sasa na wausoni. Ofisi ya kamishna wa eSafety ita toa usimamizi na utekelezaji wa marufuku hiyo, ikijumuisha kuweka hatua za busara ambazo kampuni za mtandao wakijamii zinaweza fuata kuitekeleza.
Kampuni yamawasiliano ya Optus, imelipa faini ya zaidi ya $12 milioni kwa kukiuka sheria za simu za dharura wakati wa mitandao yake ilipotea mwaka ulio pita, hali iliyo sababisha usumbufu mkubwa. Uchunguzi wa mamlaka ya vyombo vya habari na mawasiliano ya Australia ilipata kuwa, kampuni hiyo ilifeli kutoa fursa ya huduma yakupiga simu wakati wa dharura, kwa zaidi ya watu 2000 wakati wakupotea kwa mtandao huo. Kampuni hiyo ilifeli pia kufanya ukaguzi wa ustawi kwa watu 369, ambao walikuwa wamejaribu kupiga simu ya dharura wakati wa kupotea kwa mtandao hua.
Mpinzani mkuu wa Trump katika uchaguzi wa Novemba 5, Makamu wa Rais Kamala Harris alitoa hotuba ya kukubali kushindwa mbele ya maelfu ya wafuasi wake. Kwanza, kama ilivyo kwa utamaduni uliozoeleka kwenye mataifa ya kidemokrasia, Bibi Harris alimpigia simu Trump kukubali kushindwa na kumpongeza rais huyo wa zamani wa Marekani kwa ushindi aloupata utakaomrejesha ikulu ya White House kwa miaka mingine minne.
Afrika Kusini imeufunga mpaka wake na Msumbiji muda mfupi baada ya kuufungua leo, wakati ambapo ghasia za baada ya uchaguzi katika nchi hiyo jirani yake zikiendelea na kusababisha makabiliano kati ya polisi na waandamanaji. Mamlaka Afrika Kusini pia zimewatahadharisha raia wake waahirishe safari zisizo na umuhimu kuelekea Msumbiji.
Wadau wa kisiasa nchini Sudan Kusini ambao hawakuwa wametia saini mkataba wa amani wa mwaka 2018, wamekubali kuanza tena mazungumzo ya amani jijini Nairobi, baada ya miezi kadhaa ya kusuasua wakionesha kutoridhisha na mchakato wa Amani.
Hatua yao imekuja kufuatia ziara ya rais William Rutp jijini Juba wiki hii, ambapo alifanya mazungumzo na rais Salva Kiir, makamu wake Riek Machar pamoja na washirika wengine wa serikali ya mpito. Katika taarifa yake baada ya kuhitimisha ziara kwenye taifa hilo, rais Ruto amesema pande husika katika mchakato wa Amani wa Sudan, wamekubali kurejea tena kwenye meza ya mazungumzo kujadiliana masuala yaliyokuwa kikwazo.