Hata hivyo Bw Morrison ametupilia mbali mapendekezo ya makosa au kuwa alipotosha baraza la mawaziri, akisema kuwa matokeo ya ripoti hiyo yalitokana na kutoelewa kwa kimsingi jinsi serikali inavyo fanya kazi.
Mbunge wa chama cha Greens Max Chandler-Mather, amesema hatua zaidi zinatakiwa kukabiliana na dhiki yakukodisha.
Upinzani nchini Zimbabwe umekwenda mahakamani kulalamikia ukandamizaji wa serikali. Balozi Ali Karume apokonywa uanachama wa CCM, na shirika la Human Rights Watch laitaka Tunisia kuacha kuwafurusha wahamiaji wa Kiafrika.
Katika michezo Australia na Argentina za pata cha metema kuni katika mechi za kimataifa za raga, na mbichi na mbivu za bainika katika ligi za NRL, AFL na wiki ya pili ya michuano ya Wimbledon yaanza.