Taarifa za habari: Nafasi ya mwekahazina wa taifa bungeni mashakani

Mweka hazina wa Australia Josh Frydenberg

Mweka hazina wa Australia Josh Frydenberg ajipata mashakani kuhusu uraia wake Source: AAP

Mahakama imeelezwa kuwa mweka hazina wa shirikisho Josh Frydenberg, hastahili kuwa bungeni kwasababu ya uraia wa Hungary wa mamake.


Chini ya sheria ya Australia, watu wenye uraia pacha, hawawezi kuwa bungeni, kwa hiyo Bw Frydenberg amejipata akikabiliwa kwa changamoto yakisheria ndani ya mahakama, kuhusu ushiriki wake bungeni.

Waziri wa afya wa shirikisho Greg Hunt amesema abiria kutoka meli ya Diamond Princess, watafanyiwa uchunguzi wa ziada kwa virusi vya coronavirus kabla hawaja wasili nyumbani.

Tangazo la hivi karibuni la rais wa Sudan kusini Salva Kiir kwamba amepunguza majimbo nchini humo kutoka 32 hadi 10 ni tamko ambalo limepokelewa kwa hisia tofauti ndani na nje ya taifa hilo.

Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yanataka serikali ya Rwanda iruhusu uchunguzi huru na wa kina, kuhusiana na kifo cha mwanamziki maarufu wa nyimbo za injili na maridhiano nchini humo, Kizito Mihigo.


Share