Hakuna sheria zozote zinazo husiana na matumizi ya AI nchini Australia.
Uchaguzi wa shirikisho ukiwa una karibia, naibu mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya kuunda sera za teknolojia Zoe Jay Hawkins, amesema "imechelewa sana kwa mageuzi makubwa yakisheria kwa Australia" kabla tuelekee katika uchaguzi mkuu.
Hatimae ni jukumu la wapiga kura kuamua ni nini halisi na nini bandia, inapokuja kwa maudhui yanayo tengezwa kwa AI katika kampeni za uchaguzi.
Msemaji wa Tume ya Uchaguzi ya Australia Alex Morris, amesema "kuweni waangalifu ila msiogope".
"Ukiona kitu ambacho hauwezi toa dhamana ya usahihi wacho, kama hauna uhakika ni sahihi, usikichangie kabla umekifanyia uchunguzi."
Katika makala haya tuna kile ambacho wa Australia wanastahili tarajia kutoka AI tunapo elekea katika uchaguzi wa shirikisho wa 2025.
Ukiona uongo wowote au maudhui yakutilia shaka tunapo elekea katika uchaguzi mkuu, tujulishe.