Ni taarifa iliyo karibisha wiki na bila shaka ili endelea kuwa taarifa iliyo jadiliwa wiki ilipo kamilika.
Na licha yakumuunga mkono waziri mkuu wiki hii bila masharti, mweka hazina wa taifa, waziri wa nishati na waziri wa maswala ya nyumbani, wote wali kiri wana nia yaku rithi wadhifa huo.
Kila mmoja wao alikiri kuwa, iwapo fursa hiyo ita tokea, bila shaka wangependa kuwa waziri mkuu katika siku za usoni.
Kauli hiyo haishangazi kutoka kwa mwanasiasa, ila pia haifai, unapozingatia mvutano unao endelea ndani ya serikali ya mseto.