Wiki hii mjini Canberra 23Feb18

Bendera ya Australia yapepea juu ya bunge la taifa mjini Canberra

Bendera ya Australia yapepea juu ya bunge la taifa mjini Canberra Source: AAP


Naibu waziri mkuu Barnaby Joyce alijiuzulu baada ya madai ya unyanyasaji wakingono dhidi yake kuvuja.

Hayo yakiwa ni madai mapya katika wiki mbili zilizo jawa kashfa dhidi yake.

Isitoshe waziri mkuu wa zamani Tony Abbott alianza kuwakosoa mawaziri wa serikali, walipo tupilia mbali pendekezo lake kuhusu mahali ambapo viwango vya uhamiaji vina stahili sitishwa nchini Australia.

Matukio ya wiki hii, yana maana kwamba uvutio ambao serikali ilikuwa ime pata mwanzo wa mwaka huu, sasa ume potea.

Kasi yake yakisiasa ime yayuka kati ya kashfa na malumbano yaki siasa.


Share