Utafiti mpya kutoka Taasisi ya Alan Turing nchini Uingereza ilipata kuwa, “AI ilitumiwa vibaya katika chaguzi nyingi kubwa ila, kuna uhaba wa ushahidi kuwa ili athiri kwa kiasi kikubwa matokeo yoyote ya uchaguzi.”
Kama AI haiwezi shawishi wapiga kura, je ni jambo kubwa sana? Utafiti huo ulipata kuwa AI ina madhara makubwa kwa uaminifu. ‘Uaminifu kwa mfumo mpana wa demokrasia kwa kuchafua mazingira yetu ya taarifa.’
Kwa hiyo, uchaguzi mkuu unapo endelea karibia, matumizi ya AI yanastahili dhibitiwa?
Kulingana na hati ya serikali, mfumo wa udhibiti wa sasa wa Australia, haufai kujibu hatari zakipekee za AI.
Kilicho fanywa nikutoa ripoti mbili rasmi, zinazo pendekeza ‘ulinzi’ na kutoa ‘kiwango cha usalama wa AI kwa hiari.’ Na katika mwezi wa Septemba 2024, ‘sera’ ya matumizi ya uwajibikaji wa AI serikalini’ ilikubaliwa kutumiwa na sehemu kubwa ya vyombo vya madola pamoja na makampuni.
Kwa taarifa zaidi, tembelea sbs.com.au/sbsexamines.
Na ukiona taarifa yoyote potofu au, maudhui yenye shaka kuelekea katika uchaguzi wa shirikisho, tutumie barua pepe kwa anwani hii: [email protected]