Uchaguzi wa AI: Jinsi akili bandia ilivyo athiri chaguzi kubwa duniani

Factchequado.png

This TikTok account uses an avatar to spread misinformation about US immigration issues in Spanish. Credit: Source: Factchequeado

Kutoka "Kamala mkomunisti" hadi kwa uidhinishwaji wa Bollywood, akili bandia na taarifa potofu zilikuwa na nafasi kubwa katika chaguzi kubwa zaki demokrasia mwaka jana.


Kwa mara ya kwanza, maandishi yanayo tungwa kwa AI, video, picha na sauti zime tumiwa katika kampeni za kisiasa.

Nchini India, maudhui bandia ya waigizaji wa Bollywood, waki idhinisha vyama vya kisiasa vili ibuka katika kurasa za mitandao ya kijamii ya wapiga kura.

Pamposh Raina ni mchambuzi mkuu wa maudhui bandai, amesema: "Sauti zao zilibadilishwa, katika baadhi ya kesi zilibadilishwa kabisa kutoka walicho sema katika video ya asili, kufanya ionekana ni kama wana idhinisha chama fulani, wakati haikuwa hivyo."

Wakati huo huo nchini Marekani, picha iliyo undwa kupitia AI ya Kamala Harris akiwa amevaa nguo za afisa waki Soviet, ilichangiwa sana, haswa miongoni mwa wapiga kura waki Latino.

Mhariri Mkuu wa Factchequeado Ana Marìa Carrano amesema: "katika kesi ya jumuiya ya wanao zungumza Kihispania, katika kesi ya jumuiya yawatu wanao zungumza Kihispania, watu wengi kutoka ukanda wa Marekani yaki Latin wana uhusiano tofauti na tawala za kimabavu. Kwa hiyo, kuna uzoefu tofauti na kukataa ushirika wa aina hiyo."

Katika makala haya, SBS Yachunguza ina elekea India na Marekani kuchunguza jinsi taarifa potofu zilizo undwa kwa akili bandia (AI) zilivyo athiri chaguzi zao.

Share