Ni sahihi, tarehe 3 Mei itakuwa tarehe ya uchaguzi mkuu. Ila wanasiasa wame kuwa wakifanya matangazo makubwa tangu mwaka jana. Je, hatua gani itafuata sasa?
Leo, Waziri Mkuu alimtembelea Gavana Mkuu na kumuomba avunje bunge la taifa.
Kama hauta kuwa nchini siku ya kupiga kura, unaweza piga kura kwa kutumia posta, kupiga kura mapema au kupiga kura katika ubalozi wa ng'ambo. Kama yote haya nikama yana kuchanganya, usiwe na wasi wasi.
SBS itakuletea kila kitu unacho stahili jua, kabla upige kura. Unaweza fuata makala ya 'SBS Our House' kokote unako pata makala yako yaliyo rekodiwa.