Hata hivyo, moto ume unda bara la Australia kwa ma milioni ya miaka na huwa na sehemu muhimu katika usawa wa mimea na wanyama katika jamii nyingi za ikolojia barani.
Kwa maelfu ya miaka, watu wa Mataifa ya Kwanza wame linda na kusimamia ardhi hii, wakitumia moto kama kifaa muhimu.
Uchomaji mkubwa wa jadi ulikandamizwa chini ya uongozi wa ukoloni, ila leo, uchomaji wakitamaduni una pata umaarufu tena kama mfumo ulio thibitishwa kwa kupunguza mioto ya vichaka na kudumisha afya ya nchi.
Uchomaji wakitamaduni ni mazoezi ya usimamizi wa ardhi ambayo watu waki Aboriginal nchini Australia wametumia kwa ma milenia ya miaka. Ushahidi unaonesha kuwa hatua hiyo imekuwa na nafasi muhimu kwa mipango ya riziki, ulinzi wa mazingira na kuzuia moto wa nyika.
Jisajili au fuata makala yaliyo rekodiwa ya Australia yafafanuliwa kwa taarifa muhimu na, vidokezo kuhusu kuanza maisha yako mapya nchini Australia.
Je una swali lolote kuhusu au pendekezo ya mada? tutumie barua pepe kwa [email protected]