Kwa zaidi ya miaka 160, shindano hilo limevutia umati mkubwa wa watu wanao sherehekea farasi bora zaidi duniani pamoja na wanao ziendesha.
Ila, shindano hilo lime zua maswali pia kuhusu maadili ya sekta ya mashindano ya farasi, ustawi wa wanyama pamoja na kamari.
Jumanne ya kwanza ya Novemba, karibu shughuli zote nchini Australia husimama kwa muda kwa ajili yakutazama shindano la farasi. Shindano hilo lina fahamika kama 'shindano linalo simamisha taifa’.
Melbourne Cup ni kilele cha kalenda yamashindano na moja yamashindano yenye fahari zaidi duniani.