Mamilioni ya watu ambao wana viza wan wasiwasi au, wamechanganyikiwa kuhusu hatma yao.
Baadhi ya watu hao wanajumuisha watu ambao wako nchini kwa viza ya likizo, wanafunzi, familia na wachumba, wafanyakazi na viza za ujuzi, wakimbinzi, watu wenye viza zamuda mfupi na watu ambao viza zao zilifutwa, pamoja na watu wengi zaidi nahata viza za raia wa New Zealand.
Shirika la habari la SBS linakupa ushauri mpya, pamoja na msaada unao tolewa kwa watu ambao wana viza nchini.
Kama unaviza ya muda mfupi, ya aina yoyote, tembelea tovuti ya www.servicesaustralia.gov.au na ufuate hatua za malipo ya watu wenye viza.
Na unaweza pokea taarifa mpya kuhusu virusi vya korona katika lugha yako kwenye tovuti hii: sbs.com.au/coronavirus.