Content Warning:
- This article and podcast episode contain references to violence that could distress some people.
Captain James Cook alipowasili kwa mara ya kwanza katika fukwe ya nchi inayo julikana leo kama Australia, ali dai kuwa nchi hii ni 'Terra Nullius', kumaanisha si nchi ya mtu yeyote. Hata hivyo, kisiwa hiki ambacho ni bara pia, kilikuwa nyumbani kwa mamia yamataifa tofauti yawa Aboriginal na watu kutoka mataifa ya Torres Strait Islander, pamoja na ukoo. Kumaanisha tamko hilo liliwafanya mamia yamaelfu yawatu kutoka jamii za kwanza kuwa ‘mali’ ya ufalme wa Uingereza.
Hali hiyo ilikuwa kichochezi cha Frontier Wars, mugogoro mubaya kati yajamii zakwanza na wakoloni hali iliyo ashiria mwanzo wa Australia. Hiyo ni historia ambayo imeanza kutambuliwa tu hivi sasa.
Rachel Perkins ni mtengenezaji wa filamu, yeye pia ni mwanamke kutoka jamii yawa Arrernte na Kalkadoon na sehemu ya familia yake ina asili ya Ulaya. Alitengeza filamu kwa jina la “The Australian Wars”, ni filamu inayo mulika harakati zawatu wa jamii yakwanza, wakitetea nchi yao dhidi ya wakoloni kutoka Uingereza.
These were the wars that were fought in Australia and they were the wars that really made the modern Australian state.Rachel Perkins, Filmmaker
Vita vya Australia vilishuhudiwa katika bara nzima, kuanzia wakati wakuwasili kwa meli ya kwanza yawakoloni katika mwaka wa 1788, na hadi kati ya miaka ya 1930s, ila migogoro hii, haikufunzwa katika shule au hata kutambuliwa kama vita hadi mwisho wa karne ya 20.
Profesa Henry Reynolds ni mmoja wa wanahistoria wa Australia wanao heshimiwa, yeye pia ni mtaalam wa maswala yakivita. Alipo anza kufunza historia katika mwaka wa1966, palikuwa uhaba mkubwa wa taarifa kuhusu watu waki Aboriginal katika vitabu vya historia.
“Iliwataja wa Aborigines mara mbili tu, kwa kupita na hapakuwa hata taarifa yoyote ya kina”, alisema.
Tazama video fupi ya filamu ya The Australian Wars:
Prof Reynolds amesema kwa upande mmoja hii ilikuwa sababu Frontier Wars haziko onekana katika kati ya karne ya 20 kama vita kamili, kwa sababu mgogoro huo ulilinganishwa na vita vya msituni au guerrilla.
“Mtazamo ulikuwa kwamba ni vita vidogo sana na vilisambaa kuzingatiwa kuwa na uzito wa vita. Hapakuwa magwanda, wanajeshi walio tembea kwa mguu kupigana… Hapa kuwa kesi yoyote yavikosi vingi na vita vikubwa kwa hali yavita vyakitamaduni, ila hata hivyo, ni wazi ilikuwa aina ya vita.”
Dr. Nicholas Clements ni mwanahistoria na mtaalam mwingine wa the Australian Frontier Wars, naye anakubali hoja hiyo. Amesema dhana hiyo potofu ni sababu ya vita vya kwanza navya pili vya dunia, ambavyo vilibadili jinsi mapambano yakivita yanavyo chukuliwa.
Hata hivyo, aina hizi za vita kubwa, si kawaida katika historia ya binadam.
“Walijua wakati huo ilikuwa vita. Hati zote zakikoloni zilisema ni vita ila, katika karne ya 20 na 21, tumepoteza mtazamo huo. Na nadhani pia kuna sababu za chini chini zakisiasa, kwa nini watu wengi hawaitambui kama vita” Dr Clements ame elezea.

Frontier conflicts took place across the nation. Source: Supplied / Australian War Memorial
“Hatahivyo, jeshi la Uingereza lilitumia nguvu kuhakikisha ukoloni wao katika bara hili ulifanikiwa,” ameongezea.
Mabo na kupinduliwa kwa 'Terra Nullius'
The Australian Wars ziliweza tambuliwa tu baada ya tangazo la ‘Terra Nullius’ kuhojiwa nakupinduliwa katika miaka ya mapema ya 1990, katika kinacho julikana kama uamuzi mhimu wa Mabo.
“Hadi wakati huu, mtazamo ulikuwa kwamba wa Aborigine hawakumiliki ardhi yao, kwa hiyo vita havinge husu udhibiti wa ardhi kwa sababu hawakuwa na hati miliki yoyote ya ardhi hiyo. Baada ya 1992 na hukumu kutolewa, hali ya vita ilibidi ibadilike kwa sababu ilikuwa wazi ilihusu aina ya maswala ambayo vita daima hu husu kama; udhibiti wa nchi,” Prof Reynolds amesema.

Eddie Mabo with his legal team. Source: SBS
“Kulikuwa kasoro kwenye moyo wa ukoloni wa Uingereza nchini Australia. Tofauti na nchi zingine ambazo wangereza walikuwa wakoloni, hawakutambua uhuru wa wamiliki wa jadi wa hapa Australia. Kwa sababu hiyo, hapakuwa mikataba, hapakuwa jaribio lakufanya mashauriano na wenyeji na hadi leo tunaendelea kuwa na matatizo kwa upande wakisheria, kuelewa haki zao kwa ardhi ni gani.”
Nakufeli huko kushauriana, kulisababisha umwagaji damu mubaya.

Nowhere was resistance to white colonisers greater than from Tasmanian Aboriginal people, but within a generation only a few had survived the Black War. Source: The Conversation / Robert Dowling/National Gallery of Victoria via The Conversation
Nyumba ya makumbosho ya taifa ya Australia pekee, ina hifadhi zaidi yamabaki 400 yamababu waki Aboriginal, wengi wao wakionesha ushahidi wakufa kwa kunyongwa, kukatakatwa na katika mauaji yakimbari.
Rachel Perkins amesema wajukuu wa walio pona mgogoro huo watakumbuka daima.
A lot of Aboriginal people have been the vessels for carrying with history. Aboriginal people have handed down the stories of what happened to them, to us, in our families. So, I grew up knowing about the massacre of my people in Queensland and I knew about the violent rape of my great grandmother, etc.Rachel Perkins
The Black War
Jimboni Tasmania kulikuwa vita vilivyopewa jina la Black War vita hivyo vilikuwa kati ya (1824-1831) vilikuwa vita vikali zaidi katika historia ya Australia.
“Katika vita vya Black Wars watu wengi wa Tasmania wali uawa kuliko idadi yawatu wa Tasmania walio fia nchini Korea, Malaysia, Indonesia, Vietnam, na katika ujumbe wakulinda amani kwa ujumla,” Rachel Perkins amesema katika makala ya Australian Wars.
Dr Nicholas Clements ameongezea kuwa kiwango cha vurugu kutoka pande zote kilikuwa kikubwa sana, wakoloni na watu wao “walijawa hofu”.

Historian and author, Dr Nicholas Clements. Source: SBS / NITV News
In fact, serious people were contemplating having to abandon the colony.Dr Nicholas Clements, Australian Historian.
Ila wazungu walishinda, na karibu wawaangamize watu wa asili wa Tasmania.
Vita viliongezeka ukali kwasababu ya ukatili wakijinsia.
“Uchochezi wa vurugu, mshale ulio washa moto, ulikuwa ukatili wakijinsia ” Dr Clements ameongezea.
Ubakaji wakimfumo na utekaji nyara wa wanawake waki Aboriginal ulikuwa kawaida sana, kiasi kwamba amehusisha uponaji wa baadhi ya ukoo wawa Aboriginal kwa ukatili wakijinsia.
“Nikwa ncha ya nywele tu ndiyo sababu tuna baadhi yawajukuu wa waAboriginal jimboni Tasmania leo, kwa sababu walinusurika kuangamizwa kabisa, kwa sehemu kubwa kupitia vurugu,” Dr Clements amesema.

A nineteenth century engraving of an aboriginal camp - Marmocchi Source: Getty
Kukabiliana na moto kwa moto
Kuponda upinzani wa waAboriginal katika sehemu nyingi za Australia, wakoloni waliunda jeshi lapolisi la wenyeji, nikikosi kilichopewa mafunzo nakutumiwa kueneza hofu.
“Ulisajili wanajeshi wa asili na uliwatumia kama jeshi lako. Hakuna shaka jeshi hili lilikuwa mhimu kuvunja upinzani wa waAboriginal,” Profesa Reynolds amesema.
Wanaume walipewa mavazi rasmi, bunduki, na farasi. Dr Clements ana amini kuwa walipotoshwa nama afisa wazungu, ambao waliwatumia kwa ujuzi wao wakitamaduni wa waAboriginal pamoja na ujuzi wa pori.

Professor Henry Reynolds, historian and author. Credit: Dylan Rivers
Historia hii yote ni kitu ambacho Rachel Perkins amesema, ilibidi akabili wakati alikuwa akitengeza filamu ya Australian Wars.
“Nilipata taarifa iliyokuwa imerekodiwa na bibi yangu, akizungumza kuhusu familia ya mamake ilivyo uawa. Nilikuwa sijawahi sikia hadithi hiyo kabla na, nilikuwa sijawahi fika katika eneo la tukio hilo. Nilikuwa sijawahi jua ilikofanyikia, hadi nilipotengeza makala haya,” amesema.

Filmmaker Rachel Perkins says making The Australian Wars documentary was an "epic undertaking". Source: SBS
“Iwapo mababu wa mtu walihusika au la, sote ni warithi wa ardhi yawa Aboriginal, ambayo ni ardhi iliyo ibiwa. Sote tuna nafasi yakufichua historia hii, nakukubali historia hii pamoja nakuwa na nafasi kwa siku chanya ya usoni.”

Canberra, ACT, Australia - July 12, 2014: Credit: iStock Editorial
Ni kwa nini historia hii ina adhimishwa?
Profesa Reynolds ana amini kuwa Australia, taifa linalo waenzi wanajeshi walio uawa katika kumbukumbu zao nyingi za vita, inahitaji tambua kwa uwaji kuwa Frontier Wars zilifanyika na zilijawa matenda yakihalifu dhidi ya binadam.
“Ni kwa nini hatuwezi tambua vita vya Australia"? ame hoji.
“Hali hiyo haiko hivyo Marekani, wanatambua migogoro yote nawamarekani wa kwanza kama, vita rasmi. Bilashaka sivyo hivyo pia nchini New Zealand, daima vita vya wa Maori vimekuwa sehemu mhimu ya historia yao.”
Rachel Perkins amesema sababu ya dosari hiyo ni rahisi.
“Australia ni moja ya nchi zakipekee duniani, ambako wakoloni hawakuondoka,” Amesema.
The colonists or the settlers that came with them have remained in power, so I think that makes it a bit more difficult for the nation to acknowledge or celebrate those that defended the country because the colonial occupying force hasn’t left!
Dr Clements ana amani kuwa kauli ya ‘lest we forget’, ambayo hutumiwa sana kuwaenzi wanajeshi wa Australia walio fariki, inastahili tumiwa pia kwa wapiganaji walio pigana dhidi ya umiliki wa wangereza kwa ardhi zao.
“Naweza hisi fahari zaidi kama nchi yangu inatambua kwa ujasiri zama zayo binafsi, makosa yawatangulizi, pamoja nakuwa na nia yaku kosoa makosa hayo kwa siku za usoni.… Nataka watoto wangu wakuwe kama nikupitia kumbukumbu au, kama nikwa utoaji wa majina mawili, u Aboriginal uko pale, upo sasa, na unatambuliwa.”
Makala ya The Australian Wars yataoneshwa Jumatano 21 Septemba saa 7.30 usiku kwenye runinga za SBS na NITV.
Makala hayo yataweza patikana pia mtandaoni kupitia SBS On Demand katika lugha tano. Lugha hizo zinajumuisha: Kichina rahisi, Kiarabu, Kichina chakitamaduni, Kivietnam pamoja naki Korea, hali ambayo itawaruhusu wa Australia wengi zaidi kuwa na fursa yakuchangia katika mada hii mhimu. Makala hayo yataweza patikana pia kupitia sauti yenye maelezo kwa watu wenye ulemavu wakuona.