Walimu wahamiaji nchini Australia

Yongfei Lin ni mwalimu katika shule yajamii ya lugha yakimandarin mjini Sydney

Yongfei Lin ni mwalimu katika shule yajamii ya lugha yakimandarin mjini Sydney Source: Supplied

Njia yakuwa mwalimu nchini Australia kama unavyeti kutoka ng'ambo, mara nyingi huwa ngumu na inawafungia njia maelfu yawalimu watarajiwa kuingia katika mfumo.


Hiyo ni kulingana na taarifa kutoka taasisi ya lugha za jamii ya Sydney, ambayo inajaribu kubadili hali hiyo na kuwasaidia walimu ambao ni wahamiaji kutoka kote duniani, kupata hati zakufundisha katika shule za Australia.

Idadi ya walimu 100 wanatarajiwa kukubaliwa katika masomo hayo, katika mwaka huu wa 2021.


Share