Wangeci Kones alikuja Australia akiwa na matumaini yakutumia shahada yake ya masoko, katika kazi sawia na alivyo kuwa akifanya nchini Kenya.
Hata hivyo hali aliyopata nchini Australia ilikuwa tofauti na matarajio yake. Ilibidi abadili mtazamo wake kwa kazi alizotaka kwa muda, hadi alipo pata kazi iliyo endana na ujuzi na uzoefu wake.