ANC yahamasisha umoja baada yakupoteza wingi bungeni, ila yataka kusalia madarakani

Matokeo ya mwisho ya uchaguzi mkuu wa Afrika Kusini yame thibitisha mabadiliko makubwa katika nyanja ya kisiasa ya nchi hiyo.


Kwa mara ya kwanza tangu mwisho wa uongozi kwa misingi ya ubaguzi wa rangi ulio julikana kama apartheid, chama cha African National Congress (ANC) kime poteza wingi wacho bungeni.

Chama cha African National Congress, kime tawala siasa za Afrika Kusini kwa 30 iliyopita, kwa maana ya tangu kilipo ingia madarakani mwisho wa apartheid.

Ila sasa, matokeo ya mwisho ya uchaguzi mkuu wakitaifa yame rejesha matokeo muhimu: chama hicho kimepoteza wingi wacho bungeni, wapiga kura wengi wamekiacha kwa sababu ya kudorora kwa uchumi, viwango vya juu vya ukosefu wa usawa wa mapato, kupotea kwa umeme mara kwa mara pamoja na ufisadi ndani ya chama hicho.

Share