Bunge la Ulaya limeidhinisha Alhamisi maazimio ya haki za binadamu kuhusu Tanzania, na kulaani hatua ya kutiwa nguvuni mwanasiasa Tundu Lissu ambaye ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini humo Chadema. Katika azimio lao, wabunge wa Ulaya wamelaani kukamatwa kwa kiongozi huyo na kueleza wasiwasi wao mkubwa kuhusiana na tuhuma za kisiasa dhidi yake ambazo hukumu yake huenda ikawa ni kifo.
Kardinali Robert Prevost ametangazwa kuwa kiongozi ajaye wa Kanisa Katoliki. Yeye ndiye Papa wa kwanza kutoka Marekani na kuchukua jina la papa Leo XIV. Kanisa Katoliki limempata Kiongozi wake mpya, Papa Leo wa 14 atakayewaongoza takriban waumini bilioni 1.4 kote ulimwenguni. Kiongozi huyo amepatikana Alhamisi jioni baada ya uchaguzi uliofanywa na makadinali wapatao 133 kutoka mataifa 70.