Taarifa ya Habari 8 Mei 2025

Bench - Swahili.jpg

Waziri Mkuu Anthony Albanese amesema mtazamo wa mhula wa pili wa serikali ya Labor, utakuwa kuimarisha mahusiano na washiriki walio ng’ambo, kuhakikisha utulivu wa kiuchumi nyumbani.


Mageuzi kwa viwango vya chanjo vya mfamasia wa New South Wales, vitaruhusu wafamasia kutoa chanjo za mafua kwa watoto wachanga, ambao ni miongoni mwa makundi ambayo viwango vyao vya chanjo vimerudi nyuma.

Moshi mweusi umetoka kwenye chimni ya Kanisa la Sistine ishara kuwa makadinali wameshindwa kumchagua kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki katika duru yao ya kwanza ya kura ya kongamano lao.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa M23 wameanzisha tena mazungumzo ya amani huko Doha, Qatar, kama sehemu ya juhudi za kidiplomasia kumaliza mgogoro ulioathiri mashariki mwa nchi hiyo.

Katika michezo, Arsenal yatupwa nje ya michuano ya kombe la klabu bingwa la Ulaya.

Share