Taarifa ya Habari 6 Mei 2025

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Anthony Albanese ata anza muhula wake wa pili kama Waziri Mkuu akiwa na serikali ya wengi, baada ya ushindi mkubwa wa chama cha Labor, chama chake kilishinda viti 86 bungeni.


Waathiriwa wa uhalifu jimboni New South Wales hivi karibuni wata kuwa na haki yakupata taarifa mpya kuhusu hali ya walio watendea maovu wakiwa ndani ya mfumo wa kizuizi, chini ya sheria mpya.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu leo kimezindua ripoti yake ya 23 ikipewa jina la "kurejea kwa watu wasiojulikana" kufuatia kurejea kwa matukio ya utekaji na kupotea kwa watu yakifanywa na watu wasiojulikana. Akisoma maudhui ya ripoti hiyo leo, Mei 5, Kaimu Mkurugenzi wa LHRC, Fulgence Masawe amesema, hali ya haki za binadamu ilizorota kidogo kwa mwaka 2024 ikilinganishwa na mwaka 2023.

Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.

Share