Jamii zawa hamiaji zimefanyia kampeni kwa miaka mingi swala la viza zamuda mrefu, ambazo zinaweza ruhusu familia kuungana nama bibi nama babu wao ila, wahamiaji wengi wanasema wana hisi wanatengwa kupitia masharti magumu ambayo yame wekwa katika viza hiyo mpya.
Licha ya malalamishi hayo, serikali imesema kuwa viza hiyo ili undwa kupitia ushauriano na jamii, na kigezo cha mapato kipo, kuhakikisha mdhamini ana rasilimali zakutosha, kuwasaidia wazazi wake. David Coleman ndiye waziri wa uhamiaji wa shirikisho, ame eleza shirika la habari la SBS kuwa: Viza hiyo mpya itawasaida maelfu ya familia zawa Australia na, imefanikiwa kuwasilishwa na serikali licha ya upinzani unao endelea kutoka chama cha Labor.
Chama cha Labor kime kosoa sera hiyo ya chama cha mseto na, chama hicho kinatarajiwa kutangaza sera yake binafsi katika kampeni ya uchaguzi mkuu.