Baby blues au unyogovu wa uzazi? Jinsi yaku jisaidia pamoja na mpendwa wako

Babies holding hands

Credit: CC0 Creative Commons

Kama wewe ni mzazi mtarajiwa au mzazi mpya, huenda umesikia neno hili la kiingereza 'baby blues'. Maana yake ni hisia za uzoefu wa changamoto zaki hisia ambazo wanawake wanne kati ya watano hupata baada ya kujifungua.


Hata hivyo, unyogovu ni tofauti. Inaweza athiri mzazi yeyote na hutofautiana kwa ukali na muda wa dalili zake.

Katika kipindi hiki cha Australia ya Fafanuliwa, tuta chunguza huduma zinazo patikana nchini Australia kusaidia na kuwatibu wanao pitia uzoefu wa unyogovu baada yakujifungua.

Mama wapya wanaweza pitia kinacho julikana kama ‘baby blues’ katika siku za kwanza baada yaku jifungua. Hizi ni hisia zisizo furahisha ambazo kawaida husababishwa na mabadiliko ya homoni na yanaweza jumuisha; mhemuko, hisia za wasiwasi, kulia na hata kupata matatizo kulala. Ingawa ni changamoto, kawaida hisia hizi huisha haraka bila kuhitaji matibabu.

Hata hivyo, kama dalili zako zina endelea au zina ingilia uwezo wako wakufanya kazi kawaida, na mtoto wako mpya, unaweza kuwa unapitia uzoefu wa unyogovu baada yakuzaa.

Share