Ila nini hufanyika iwapo wewe au mpendwa wako haridhiki na huduma anayo pokea?
Haki zilizowekwa kisheria ambazo zinalinda watumiaji wanaopokea huduma za ruzuku za utunzaji wa wazee, zimewekwa wazi katika mkataba wa haki za matunzo ya wazee, chini ya Sheria ya utunzaji wa wazee ya 1997.
Haki mbili za kwanza kati ya hizo haki 14 za huduma yawazee katika mkataba huo, inajumuisha haki zakutunzwa kwa utu na heshima, nakufurahia huduma ambazo ni salama na ubora wa juu.
Ulinzi mwingine ni haki yakutoa malalamishi bila kuadhibiwa, na malalamishi yako kushughulikiwa kwa haki na haraka.
Kuzungumza na mwana harakati wa utetezi wa huduma ya wazee, pigia simu namba yakitaifa ya watetezi wa huduma ya wazee 1800 700 600 (bure bila malipo)
Kama unataka wasiliana na tume ya usalama na huduma ya ubora wa utunzaji wa wazee, piga simu kwa namba hii: 1800 951 822.