Katika baadhi ya kesi, kunaweza kuwa pia misingi halali yaku zuia uhuru wa mfanyakazi kufuata dini yake. Iwapo unazingatia kuwasilisha malalamishi kwa mamlaka husika au, kufuatilia swala hilo kisheria, ni muhimu kujua chaguzi zako kama umepitia uzoefu wa ubaguzi wakidini kazini.
Australia ni mshiriki wa mkataba wa kimataifa wa haki za kiraia na kisiasa, ambayo hutoa ulinzi mkubwa kwa uhuru wakidini, pamoja na udhihirisho wake.
Hata hivyo, michakato yaku anzisha muswada wakutoa kinga dhidi ya ubaguzi wakidini bado ina endelea. Kwa hiyo, hakuna sheria moja Australia yenye masharti kuhusu jinsi yakutumia haki zakidini.
Katika muktadha wa ajira, kuna kinga kitaifa dhidi ya ubaguzi kwa misingi ya kidini chini ya sheria ya Fair Work Act 2009, ila sheria hizo ni ndogo kwa upeo.