Idadi yawa Australia wanao kosa kuwaona ma GP yaongezeka kwa sababu ya gharama kubwa za miadi

Medicare Bulk Billing

Medicare Bulk Billing Credit: Medicare

Wakati mfumo wa huduma ya afya kwa wote ya Australia Medicare ina sherehekea miaka 40, data mpya imeonesha kuwa wagonjwa wana endelea kuepuka kuwaona madaktari kwa sababu ya gharama kubwa za miadi.


Hali hiyo ina jiri wakati serikali inasherehekea ongezeko dogo kwa wagonjwa wanao tembelea ma GP wanao toa huduma bila kuwalipisha kote nchini, baada ya serikali kuongeza zawadi mara tatu ya huduma ya Medicare bila malipo kwa wagonjwa mwisho wa mwaka jana.

Ni mwaka wa arobaini wa Medicare, urithi wa Labor ulio wasilishwa kufanya huduma ya afya rahisi, bei nafuu na kwa haki iwezekanavyo. Medicare ni mfumo wa huduma ya bima ya afya kwa wote ya Australia.

Mfumo huo huwaruhusu wa Australia na baadhi ya wageni kutoka ng'ambo, kupata huduma kadhaa za afya na hospitali kwa gharama ndogo au bila gharama yoyote.

Ila ripoti ya tume ya tija imebaini kuwa idadi yawatu wanao wanachelewesha au ambao hawa hudhurii miadi yao kwa sababu bei ime ongezeka mara mbili, kutoka 3.5% hadi 7% katika muda wa miezi 12.

Share