Waziri Mkuu ametangaza baraza lake la mawaziri, Michelle Rowland amepewa hadhi yakuwa mwanasheria mkuu wa taifa. Anne Aly amejumuishwa katika baraza la mawaziri, atakuwa waziri wa biashara ndogo, maendeleo yakimataifa na maswala ya tamaduni nyingi. Waziri wa Afya Mark Butler ata ongezwa jukumu laku simamia mfumo wa bima ya walemavu maarufu kwa jina la NDIS, baada ya kustaafu kwa Bill Shorten aliyekuwa waziri wa NDIS.
Waafrika kusini wazungu 49 wanaodai kuandamwa kutokana na rangi yao,Afrika Kusini, wapewa hifadhi nchini Marekani kwa pendekezo la rais Trump. Kundi la kwanza la Waafrika kusini wazungu 49, waliodai kubaguliwa kutokana rangi yao na kisha kupewa hadhi ya ukimbizi nchini Marekani chini pendekezo la rais Donald Trump,wamesafiri kuelekea Marekani. Afrika Kusini imesema Marekani imejiingiza kwenye suala la ndani la kisiasa la nchi yake ambalo hailifahamu.
Watu zaidi ya 100 wamethibitishwa kupoteza maisha kufuatia mafuriko makubwa yaliyotokea usiku wa Jumamosi katika kijiji cha Kasaba, kilichoko wilaya ya Fizi, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Tukio hilo lilisababishwa na mvua kubwa iliyonyesha kwa muda mrefu, ikisindikizwa na upepo mkali, na kusababisha maporomoko ya ardhi yaliyozikwa baadhi ya nyumba.