Wakati mvuo kali zimesababisha mitandao ya mito kufurika mara kadhaa, baadhi ya jumuia katika maeneo ambayo huathirika kwa mafuriko yamepata uharibifu mkubwa kwa miundombinu, nyumba na hata kupotezwa kwa maisha.
Kwa hiyo tunaweza jua vipi kama tukio kubwa la hali ya hewa linakaribia na, unastahili fanya nini kujiandaa? Nani unaweza omba msaada? na je unastahili baki au ondoka katika sehemu hiyo?
Dhoruba na mafuriko vinapo gonga, jamii nyingi nchini Australia hutegemea misaada kutoka shirika za dharura za eneo wanako ishi.
Mashirika hayo hujulikana kawaida kama SES, mashirika haya husaidia jamii kufanya maandalizi ya dharura, kupunguza hatari kwao. Huwa wana saidia katika shughuli zakuokoa na, kufanya usafi na majukumu yaukarabati mvua inapo isha na maji yanapungua.
Nimuhimu pia kuhakikisha sera yako ya bima bado iko sawa na inafaa. Hakikisha inakupa kinga kwa aina ya matukio katika sehemu unako ishi. Hizi zinaweza jumuisha mafuriko ya ghafla, maji ya mafuriko, yanayo husiana na mmonyoko wa ardhi na, uharibifu ulio sababishwa na miti pamoja na vitu vingine vilivyo anguka.