Katika makala haya ya mwongozo wa makazi, tutachunguza jinsi yakujua kama umepoteza hela zako za uzeeni na jinsi yakuzirejesha.
Pia, nini hufanyika kwa mfuko wako wa hela za uzeeni, ukihamia ng'ambo au kifo kitakapo tokea?
Malipo ya uzeeni au, 'super', ni hela zinazo wekwa kwando na mwajiri wako katika wakati ambao unafanya kazi, ili zikusaidie kumudu maisha utakapo staafu.
Ni lazima kwa mwajiri wako aweke asilimia ya mapato yako katika akiba yako ya super, na kampuni yako ya super huwekeza hela hizo hadi unapo staafu.
Nchini Australia, kuna hatua zakuhakikisha watu hawapotezi hela zao za super, hatakama akaunti zao hazija tumiwa kwa muda.
Kama taarifa zako zamawasiliano zimebadilika na kampuni ya super haiwezi wasiliana nawe, wanatakiwa hamisha super ambayo haija daiwa kwa ofisi ya kodi ya Australia (ATO).