Katika makala ya leo tutachunguza baadhi ya faida na vipengele vya mfumo wa Medicare, na jinsi unavyo tumika pamoja na Mpango wa Faida za Dawa kutoa punguzo nyingi.
Medicare hutoa ruzuku kwa huduma nyingi mhimu zamatibabu, zinazo jumuisha kumwona daktari, vipimo vya damu, scans, x-rays, na baadhi ya upasuaji. Mfumo huo hufunika pia vipimo vya macho vya kila mwaka kwa daktari wa macho, pamoja na chanjo za watoto.
Medicare hufanya kazi pamoja na mpango wa faida za dawa au (PBS), ambao hutoa punguzo kwa dawa ambazo daktari ameshauri zitumiwe.