Siku hiyo ya huzuni huadhimisha kampeni ya Gallipoli katika vita vya kwanza vya Dunia, pamoja na wanajeshi wa Australia na New Zealand walio pigana katika migogoro iliyofuata na wanao endelea kuhudumu katika majeshi leo.
Zaidi ya idadi ya watu elfu 32 walijumuika katika sehemu ya kumbukumbu ya vita ya Australia jua lilipo chomoza mida ya Alfajiri katika siku ya ANZAC, kuwaenzi wale ambao wame hudumu katika vita vya kale na vya sasa.
Ibada hiyo ya kitaifa ni moja ya mamia ya mikusanyiko kote nchini Australia, yakuadhimisha miaka 109 yakutua kwa wanajeshi wa Australia na New Zealand katika pwani ya Gallipoli.