Mwanya wa kisheria unao ruhusu uongo wakisiasa wakati wa uchaguzi

Advance Australia sign depicting ACT independent Senate candidate David Pocock as a "Greens superman"

Advance Australia sign depicting ACT independent Senate candidate David Pocock as a "Greens superman" Source: Twitter / Twitter / David Pocock

Baada ya tarehe ya uchaguzi kutangazwa kuwa 3 Mei, kampeni zime anza rasmi. Ila matangazo ya kisiasa yame kuwa yaku sambazwa kwa miezi kadhaa. Je, unaweza amani wanavyo sema?


Kuna mwanya katika sheria ya Uchaguzi inayo ruhusu matangazo yakupotosha kusambazwa nje ya muda wa kampeni ya uchaguzi.

Wataalam wanasema hali hiyo hu sababisha uharibifu, si tu kwa sifa ya mgombea wa kisiasa ila pia kwa mchakato wakisiasa.

Katika mwaka wa 2022, Seneta huru wa ACT David Pocock aliwasilisha lalamishi rasmi kwa Tume ya Uchaguzi ya Australia (AEC) kuhusu picha yake iliyo badilishwa kidijitali, iliyo onekana mwezi mmoja baada ya tarehe ya uchaguzi kutangazwa.

Picha hiyo ili onesha Pocock akichana shati yake nakuonesha nembo rasmi ya chama cha Greens na, ilipatwa katika mabango yanayo wekwa barabarani, pamoja na kwenye ma lori yaliyo kuwa yame egezwa karibu ya vituo vyakupigia kura.

Mabango hayo yali idhinishwa na kikundi cha ushawishi chaki hafidhina kwa jina la Advance Australia.

Shirika la AEC lili amua kuwa picha hiyo ilikuwa yakupotosha na haistahili oneshwa wakati wa kampeni ya uchaguzi. Advance Australia haiku kubaliana na matokeo hayo ya AEC ila, ilikubali kuto onesha picha hiyo tena.
dyson_ad.PNG
Digitally altered flyers of Alex Dyson, authorised by Advance Australia, were placed in voter's mailboxes throughout the candidate's electorate of Wannon. Credit: Supplied
Tarehe 31 Machi taarifa ilitolewa kwa uchaguzi wa shirikisho wa 2025, hatua ambayo ili anzisha rasmi kampeni za uchaguzi mkuu.

Kwa hiyo Advance Australia ilipo amua kusambaza picha zilizo badilisha kidijitali Februari mwaka huu, wakati huu ikitumia sura mpya, hawaku vunja sheria yoyote.

Katika eneo bunge la Wannon, picha iliyo badilishwa kidijitali ya mgombea huru Alex Dyson ilichangiwa katika mabango ikimuonesha akichana shati yake nakufichua nembo rasmi ya chama cha Greens.

Bw Dyson alisema picha hiyo ime zua hisia mseto.

“Baadhi bila shaka wali shangaa walio kuwa makini naku weza ona kuwa ilikuwa kazi ya Advance Australia. watu wengine, ambao pengine hawaoni vizuri, au hawakusoma maandishi kwenye bango vizuri, wali shangaa pia kwa sababu tofauti.
It’s pretty wild.
Profesa Mshiriki katika shule ya Sheria ya Chuo cha Monash Yee-Fui Ng amesema Advance Australia "wame ambiwa tendo hili hali ruhusiwi na wame pata tu mwanya katika sheria.”

Msemaji wa Advance Australia ali eleza SBS Examines kuwa AEC ili washauri kuwa taarifa kama bango la Bw Dyson “hali kiuki sheria ya uchaguzi.”

Kitengo 329 cha Sheria ya Uchaguzi inapiga marufuku uchapishaji wa taarifa ambazo zina weza potosha au danganya mpiga kura ila, sheria hiyo huanza kutumika tu wakati taarifa kuhusu uchaguzi inapo tolewa.

Bill Browne ni Mkurugenzi wa, Taasisi ya Demokrasia na Mradi wa Uwajibikaji nchini Australia. Amesema jukumu la mtazamaji kuamua kinacho potosha inapokuja kwa matangazo ya kisiasa.

“Daima ni vizuri kuwa na kiasi fulani cha mashaka, wakati wakutathmini matangazo na, pengine hali hiyo huwa mara mbili kwa matangazo ya kisiasa.”

Share