Maandalizi yanayofaa yatapunguza uwezekano wakupotea. Ila kama unapotea, utayari utaongezea uwezekano wako kupatwa.
Kutembea msituni ni shughuli maarufu ya burudani nchini Australia. Ni moja ya njia bora yakugundua mazingira makubwa naya kipee ya nchi hii.
Licha ya juhudi bora za kila mtu, watu hupotea wakitembea msituni.
Takriban 95% yao hupatikana ndani ya masaa 12 na watu wenye ujuzi wa mazingira ya nje kama Caro Ryan, yeye ni kamanda wa watafutaji na waokoaji katika shirika la NSW SES Bush Search and Rescue.