Polisi wamesema mshambuliaji aliyehusika katika shambulizi hilo, alikuwa ni mwanaume mwenye miaka 40, mwenye matatizo ya afya ya akili na hana uhusiano wowote na ugaidi.
Wakaaji wa Sydney wana endelea kukerwa baada ya shambulizi katika moja ya soko kubwa mjini humo mchana wa Jumamosi 13 Aprili, ambako watu sita wali uawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Mwanaume mmoja ali ingia ndani ya soko la Westfield Bondi Junction mida ya saa 9:20 mchana na, kuanza kudunga waemeaji kwa kisu, nakutengeza mazingira ya machafuko.
Jeshi la Polisi la New South Wales liliwasili katika sehemu ya tukio na hatimae afisa wa jeshi la polisi alipiga risasi naku muuwa, baada ya onyo kadhaa kwa mwanaume huyo ajisalimishe.
Waziri Mkuu amesema amepokea salamu za pole kutoka kwa viongozi wa dunia usiku wakumakia, ambao walikemea tendo hilo la vurugu.
Kasri ya Buckingham nayo ilitoa taarifa ambako Mfalme Charles III na mkewe Camilla, wali elezea huzuni yao kwa shambulizi hilo la kisu.
Naye waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak, Rais wa Marekani Joe Biden na Papa, walituma salamu za ushikamano kwa familia zilizo athiriwa kwa shambulizi hilo.