Waziri wa maswala ya kigeni wa Australia Penny Wong pamoja na Waziri wa Ulinzi Richard Marles, ni wenyeji wa mkutano na washirika wao kutoka New Zealand mjini Melbourne. Mkutano wa kwanza wa mawaziri wa kigeni na ulinzi wa Australia na New Zealand, unao julikana pia kama ANZMIN, unalengo wakuimarisha uhusiano waki usalama kati ya nchi hizo mbili. Ni mara ya kwanza kwa mawaziri hao kukutana, tangu pawe mabadiliko katika serikali ya New Zealand mwaka jana.
Afrika Kusini kupitia waziri wake wa Mambo ya Kigeni Naledi Pandor, imesema Jumatano kwamba Israel imekaidi uamuzi wa wiki iliyopita kutoka mahakama ya Umoja wa Mataifa, kwa kuendelea kuuwa mamia ya raia ndani ya muda wa siku chache huko Gaza. Taifa hilo pia limehoji ni kwa nini hati ya kukamatwa kwa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu haijatolewa, kupitia kesi tofauti iliyowasilishwa mbele ya mahakama ya ICC.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, Pandor amesema kwamba Afrika Kusini inatadhmini kupendekeza hatua mbadala kwa jumuia ya kimataifa, ili kushinikiza Israel kusitisha mauaji ya raia kwenye vita vyake vya Gaza dhidi ya wanamgambo wa Hamas, ingawa hakutoa maelezo zaidi.
Takribani watu 400 wamekufa kwa njaa katika mikoa ya Tigray na Amhara nchini Ethiopia katika miezi ya hivi karibuni. Takwimu hizo zimetolewa na taasisi ya taifa inayofuatilia utawala bora. Maafisa katika mikoa ya Tigray na Amhara walikuwa wameripoti katika wilaya za mikoa hiyo, lakini serikali ya shirikisho ya Ethiopia ilisisitiza ripoti hizo si za kweli.
Serikali ya Kenya imetangaza kuwa kuanzia wiki ijayo itaandama wamiliki wa vyumba vya malazi visivyosajiliwa na hata vile vinavyotumia mtandao wa Airbnb kuendesha biashara hiyo. Hii ni kufuatia ongezeko la visa vya mauaji ya kinyama yanayotekelezwa katika vyumba hivyo kote nchini katika siku za hivi karibuni.
Kwenye taarifa ya pamoja waliyoituma kwa vyombo vya habari Jumatano jioni, Katibu katika Wizara ya Usalama Raymond Omollo, Katibu wa Wizara ya Jinsia Anne Wang’ombe, Beatrice Inyangala (Elimu ya Juu) na John Olultuaa (Utalii), operesheni dhidi ya vyumba hivyo visivyosajiliwa itaanza Februari 5, 2024.
Katika michezo,
Miongozo mipya ya mtikisiko wa ubongo, zime wasilishwa kusaidia kuwalinda wachezaji chipukizi nchini Australia. Miongozo hiyo, iliyo tangazwa mapema leo Februari mosi na maafisa wa matibabu na michezo, wamejumuisha itifaki yakurejea kucheza yenye lengo laku hakikisha muda wa mapumziko ya wiki tatu kati yakisa cha mtikisiko wa ubongo na kurejea kucheza tena. Miongozo hiyo, iliundwa kwa ushirikiano kati ya mashirika kama Australian Institute of Sport, Sports Medicine Australia pamoja na mashirika mengine, ambayo yame tumia taarifa mpya na ushahidi kwa mtikisiko wa ubongo miongoni mwa wachezaji, wazazi, walimu, pamoja na wafanyakazi wa huduma ya afya.