Uvutio wa chama cha Labor katika eneo bunge hilo katika mwaka wa 2022 ulikuwa asilimia 10.9 katika uchaguzi wa jimbo hilo ila kwa sasa ushawishi huo umepungua hadi asilimia 0.6.
Waakazi wa vijijini na kanda la Australia watakuwa chini ya viwango vipya vya bei ya bidhaa 30 muhimu, zinazo jumuisha bidhaa kama unga, maziwa, na matunda. Hiyo ni sehemu ya hatua zinazo tangazwa na serikali ya shirikisho leo, kama sehemu ya jibu kwa viashirio vyaku ziba pengo, kwa pengo katika afya na ustawi kati ya wa Australia wa asili na wa Australia wasio wa asili.
Wanaharakati wa vijana wamekaribisha rasimu ya sheria ambayo ita amuru maamuzi ya serikali yazingatie maslahi ya muda mrefu yawa Australia wa sasa na wa siku za usoni. Mbunge huru Dr Sophie Scamps anatarajiwa kuwasilisha muswada huo hii leo bungeni, unao ongezwa na shirika la vijana lisilo la faida kwa linalo julikana kwa jina la, Foundations for Tomorrow.
Katika hatua mpya ya kutafuta amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) wamefikia maamuzi yatakayosaidia kurejesha utulivu katika eneo hilo linalokumbwa namzozo wa muda mrefu. Akisoma maazimio ya Mkutano huo Katibu Mkuu wa EAC, Veronica Nduva alisema mkutano umeamua kuwa pande zote zinazozozana katika mgogoro huo zisitishe mapigano mara moja na kuweka silaha chini bila masharti yoyote.
Sam Nujoma ambaye aliongoza mapambano ya miongo mitatu ya kupigania uhuru wa Namibia kutokea Afrika Kusini yenye ubaguzi wa rangi, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95, ofisi ya rais ilitangaza Jumapili. Kiongozi wa kundi la ukombozi la SWAPO alifariki Jumamosi jioni baada ya kulazwa hospitali kwa wiki tatu, akipambana na ugonjwa ambao “hakuweza kuupona”, Rais wa Namibia Nangolo Mbumba alisema katika taarifa.