Taarifa ya Habari 10 Mei 2024

Mamia yawa fungwa wa uhamiaji wanaweza achiwa huru kutegemea na hukumu ya mahakama kuu, inayo tarajiwa kutolewa leo kwa changamoto yakisheria iliyo wasilishwa na muomba hifadhi kutoka Iran.


Kiongozi wa chama cha Greens Adam Bandt ametishia chama chake hakita unga mkono sera ya nishati ya serikali ya shirikisho. Hatua hiyo imejiri baada ya tangazo la Alhamisi Mei 9 kuwa Australia itaongeza miradi ya gesi kama sehemu ya mkakati wake wa gesi ya baadae, akisema inahitajika kutekeleza ongezeko ya mahitaji. Waziri wa Rasilimali Catherine King amesema mkakati huo utaendana na mabadiliko ya serikali kwa uzalishaji sufuri wa hewa chafu kufikia 2050 ila, ilifichuliwa kuwa uchimbaji wa gesi utaweza endelea hata baaada ya tarehe hiyo. Uamuzi huo umepokewa kwa ukosoaji mkali, wanaharakati wa mazingira wamesema mkakati huo umefeli kushughulikia vyakutosha nakujibu janga la mazingira.

Ripoti mpya ya Deloitte kwa baraza la wanachama wa Super, imesema pendekezo la upinzani kuwaruhusu wanao nunua nyumba ya kwanza kutumia hela zao zakustaafu kununua nyumba, inaweza ongeza takriban $2.5 bilioni kwa mwaka katika bajeti ya shirikishio kufikia mwisho wa muongo. Muundo huo mpya ume onesha pia kuwa mpango huo unaweza walazimisha watu wengi zaidi kutegemea hela za ustaafu kwa sababu ya matokeo yakupungua kwa fedha za kustaafu. Baraza la wanachama wa Super, limesema sera hiyo itaweza lazimisha bei za wastan za nyumba kuwa takriban asilimia 9.5 juu katika miji mikuu.

Marais wa nchi tano za Afrika na wakuu wa serikali wamehudhuria mkutano wa Kilele wa kujadili ubora wa udongo na mbolea barani Afrika, wakitoa wito wa uwepo wa mkakati wa pamoja, hatua za pamoja na uwekezaji ili kuiwezesha Afrika kuzalisha chakula cha kutosha. Mkutano huo unaofanyka jijini Nairobi unahudhriwa na marais wa nchi tano za Afrika akiwemo Hakainde Hichilema wa Zambia, Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe, Nangolo Mbumba wa Namibia, Dkt Lazarus Chakwera wa Malawi na Faustin-Archange Touadéra wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, pamoja na mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat. Katika mktano huo rais Hichilema wa Zambia amesema inastaajabisha kuwa mataifa mengi ya Afrika bado yanaendelea kuagiza kwa wingi mbolea kutoka mataifa ya nje licha ya uwezo wake wa kujitegemea kuzalisha chakula cha kutosha, na kutoa wito kwa mataifa ya Afrika kufanya biashara kwa pamoja ikiwa ni sehemu ya kuinua uwezo wa nchi husika katika uzalishaji wa chakula. Rais wa Kenya William Ruto ameeleza kuwa ni sharti Afrika ijitahidi kupata mbolea ya bei nafuu, bora na inayoweza kupatikana kwa urahisi kwa utengenezaji wa ndani ya mataifa ya Afrika, hatua ambayo itaongeza tija na uzalishaj na kufanya Afrika ijitosheleze kwa chakula.

Mgomo wa siku 56 wa madaktari katika hospitali za umma nchini Kenya, hatimaye wafikia muafaka, baada ya kufanya makubaliano na serikali siku ya Jumatano, na kutia saini mkataba wa kurejea kazini mara moja licha ya kutofikia muafaka kuhusiana na mishahara ya madaktari wanafunzi. Muungano wa Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno KMPDU ambao unawakilisha zaidi ya madaktari 7,000, umetangaza kufikia muafaka katika utekelezaji kamili wa mkataba wa pamoja wa maafikiano wa mwaka 2017. Na hivyo kuumaliza mgomo huo baada makubaliano yaliyotiwa saini kwenye ukumbi wa Jumba la Kimataifa la Mikutano la Kenyatta, KICC, jijini Nairobi.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alielezea kuwa ni uhaini kwa hatua ya tangazo la kampeni la chama cha upinzani ambalo linaonyesha bendera ya taifa inayowaka moto, huku uhasama kati ya vyama vya siasa ukiongezeka wiki tatu kabla ya uchaguzi mkuu.
Tangazo la kampeni lililotolewa siku ya Jumatatu na chama cha Democratic Alliance linatumia bendera inayowaka kama alama ya kile inachosema ni hatari kubwa ya chama tawala cha African National Congress kubakia madarakani katika muungano na vyama vya mrengo wa kushoto. "Nadhani ni uhaini," Ramaphosa aliwaambia waandishi wa habari wakati wa ziara yake katika jimbo la Limpopo. "Ni kitendo cha kisiasa kibaya zaidi ambacho mtu yeyote anaweza kukitekeleza," alisema, akishutumu DA kwa kunajisi ishara ya umoja wa kitaifa.

Share