Taarifa ya Habari 12 Aprili 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Kiongozi wa upinzani Peter Dutton ametetea kauli yake, yakufananisha umuhimu kwa jamii maandamano yanayo unga mkono wapalestina katika jengo la Sydney Opera House na mauaji ya halaiki ya Port Arthur.


Makampuni yamasoko madogo yana kabiliana na maswali kuhusu jinsi yanavyo weka bei za bidhaa, nakutumia nguvu zao sokoni yanapo washughulikia wauzaji. Aldi, Metcash na Endeavour wamefika mbele ya kikao cha seneti unao fanya uchunguzi kwa uwekaji bei na matendo ya ushindani wa masoko mawili makubwa ya Australia, Woolworths na Coles. Uchunguzi huo una ongozwa na chama cha Greens, wakati kuna madai yakujinufaisha kwa makampuni na kuongezewa bei kwa watumiaji na wauzaji. Uchunguzi huo una endelea.

Vituo ziada sita vya reli vime ongezwa katika mipango ya serikali ya NSW, kwa ajili yaku kabiliana na mgogoro wa nyumba. Vituo vya reli katika maeneo ya kusini magharibi ya Sydney, vitongoji vya Newcastle na Central Coast, kwa sasa ni sehemu ya mpango wakujenga nyumba mpya ndani ya mita 400 ya vituo hivyo. Mageuzi hayo ni upangaji mkubwa zaidi wa ardhi katika historia ya Sydney, na ime ahidi kutoa zaidi ya nyumba 170,000 katika maeneo ya jiji la Sydney.

Wasafiri wa anga wame epushiwa usumbufu wakati wa likizo ya shule baada ya wazima moto wa usafiri wa anga kufuta mgomo walio kuwa wame panga. Chama cha Muungano wa wazima moto wa Australia, kimetangaza kuwa wazima moto wa usafiri wa anga, wamefikia makubaliano na shirika la Airservices Australia, kukataa hitaji la kuchukua hatua hiyo. Mgomo ulio kuwa umepangwa kwa masaa manne kuanzia saa kumi na mbili asubui ya Jumatatu hauta endelea.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Israel inaendeleza vita vyake Gaza lakini pia inajiandaa kwa matukio mengine, wakati kukiwa na wasiwasi kuwa Iran inajiandaa kuishambulia Israel. Akizungumza baada ya ziara yake katika kituo cha jeshi la angani cha Tel Nof kusini mwa Israel, Netanyahu amesema wako tayari kwa yeyote atakayeidhuru Israel.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amevunja kimya chake kuhusu mgomo wa madaktari kwa kuitaka serikali ishughulikie matakwa yao ili warejee kazini. Waziri huyo mkuu wa zamani Alhamisi Aprili 11, 2024 alisema raia masikini wasioweza kumudu gharama ya huduma za matibabu katika hospitali za kibinafsi ndio wanaumia baada ya mgomo huo kuathiri huduma katika hospitali za umma.

Nyota wa zamani wa Ligi ya Mpira wa Marekani NFL na mcheza filamu ambaye alifutiwa mashtaka ya mauaji ya mkewe na rafiki yake wa kiume katika kesi iliyoteka Marekani na dunia amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 76. O.J. Simpson amefariki baada ya kuugua ugonjwa wa saratani, kwa mujibu wa taarifa ya familia yake kwenye akaunti yake ya X.

Share