Mfumo wa chama cha Labor wa "kusaidia kununua" nyumba, unapashwa wasaidia wa Australia elfu 40 kununua nyumba yao ya kwanza, wakiwa na mchango wao binafsi wa hadi 40%.
Serikali ya Queensland inatarajiwa kuwasilisha sheria zinazo piga marufuku uuzaji wa visu na silaha kwa watu wenye chini ya miaka 18, katika jibu kwa ongezeko la tatizo la uhalifu wa vijana. Kufuatia ongezeko la uhalifu kwa visu, Huduma ya jeshi la polisi la Queensland imeomba mamlaka ya ziada kufanya msako wa silaha bila kibali.
Marufuku kamili ya moto yame wekwa kwa sehemu nyingi za Victoria, jimbo hilo linapo jiandaa kukabiliana na mazingira ya kwanza ya moto tangu tukio la moto wa Black Summer la 2019 hadi 2020. Ofisi ya utabiri wa hewa imesema nyuzi joto katika eneo la Mildura inaweza fika nyuzi joto 41 na "janga" la hatari ya moto katika kanda ya Wimmera,"hali itakuwa mbaya sana" Mallee na "hatari yajuu" kwa sehemu zingine za jimbo hilo. Eneo la East Gippsland, ambako hali ya janga ilitangazwa katika mioto ya 2019, ni kanda pekee jimboni humo lenye onyo la "wastan".
Mashambulizi ya yanga ya Israel Jumatatu yamedondosha makombora kwenye mji wa Rafah na kuuwa takriban watu 70, kulingana na maafisa wa afya wa Ukanda wa Gaza, ambapo tayari kuna takriban wakazi milioni 1.4 waliotoroka kutoka maeneo mengine ya Gaza ili kuepuka mapigano.
Kikosi cha Dharura cha Sudan RSF kinatuhumiwa hivi sasa kusitisha huduma za mawasiliano na hivyo kuharibu usambazaji wa misaada na kuzusha hofu miongoni mwa wakazi takribani milioni 50 kuwasialiana na jamaa zao walioko nje ya nchi. RSF imekuwa ikipambana na jeshi la Sudan kutaka kuitawala nchi hiyo tangu April mwaka 2023, katika vita ambavyo vimesababisha vifo vya maelfu ya raia, mamilioni kupoteza kazi na kuzusha janga la njaa.
Polisi katika mji mkuu wa Kinshasa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamefyatua gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji ambao wamechoma matairi ya gari na bendera za Marekani na Ubelgiji karibu na ubalozi wa nchi za Magharibi na ofisi za Umoja wa Mataifa. Waandamanaji wanashutumu nchi za Magharibi kwa kuisaidia nchi jirani ya Rwanda ambayo inalaumiwa kwa kusaidia uasi unaoongozwa na kundi la M23 la watutsi mashariki ya nchi.