Taarifa ya Habari 14 Juni 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Maelfu ya wahamiaji waliokuwa wakitarajia kujisajili katika vyuo vya Australia, hawata weza tena kuomba viza wanazo hitaji.


Maelfu ya wahamiaji waliokuwa wakitarajia kujisajili katika vyuo vya Australia, hawata weza tena kuomba viza wanazo hitaji. Kuanzia 1 Julai, watu walio hitumu masomo ya muda, wageni, wafanyakazi wa baharini na viza zingine, hawataweza omba viza za wanafunzi wakati wako nchini Australia. Idara ya Maswala ya Nyumbani imesema watu wenye nia halisi yakusoma, bado wataweza omba viza kutoka nje ya Australia. Mageuzi hayo yana lengo laku kabili hatua za "kuhama hama kutoka viza", ambayo idara hiyo imedai imechangia kwa ongezeko la kundi la kile inacho ita "kudumu kwa muda" la wanafunzi waki mataifa wa zamani nchini Australia.

Viwango vya ukosefu wa ajira nchini Australia vili pungua tena mwezi ulio pita, hali hiyo ikimulika wafanyakazi wanao rejea kazini baada ya idadi kubwa isiyo kawaida ya wafanyakazi walio kuwa wakisubiri kuanza kazi mpya au kurejea kazini Aprili. Kurudi nyuma kwa asilimia 4 katika mwezi Mei kutoka asilimia 4.1 katika mwezi kabla iliendana kwa upana na matarajio na mapendekezo ya uvumilivu wa kudumu katika soko la ajira, hata wakati kasi ya uchumi imepungua sana. Kulingana na ofisi ya takwimu ya Australia, tabia mbaya zinaweza kuelezea kwa sehemu kupungua kwa viwango vya ukosefu wa ajira na juu kidogo ya utabiri wa ajira 39,700 zilizo undwa. Waziri wa Ajira na mahusiano ya kazi ya Australia, Tony Burke, amesema serikali ya Labor imefikia lengo hili katika muda mfupi kuliko serikali iliyopita.

Data ya nyumba ya kampuni ya CoreLogic imeonehsa kuwa bei za nyumba katika miji ya Perth, Brisbane na Adelaide ina ongezeka haraka zaidi kuliko miji mingine kama Melbourne na Hobart. Ripoti kutoka kampuni hiyo imesema kuwa thamani za nyumba kitaifa zimeongezeka kwa zaidi ya asilimia 35, tangu janga lilipo anza 2020 ila, ukuaji hauja sambaa kwa usawa. Ongezeko z bei katika miji ya Perth, Brisbane na Adelaide imepita sana ukuaji katika vituo vingine vya miji vinavyo jumuisha Hobart, Melbourne, Canberra, Darwin na Sydney. Perth imepata ukuaji wa asilimia 62.6 ya thamani ya mali katika muda huo, kulinganisha na ongezeko la asilimia 11.2 mjini Melbourne.

Chama cha upinzani nchini Afrika Kusini Inkatha Freedom Party Jumatano kimetangaza kuwa kitashirikiana na chama tawala cha African National Congress (ANC) huku ANC kikijaribu kuunda serikali ya muungano itakayoweza kuongoza baada ya uchaguzi wa Mei 29. Bunge jipya linatarajiwa kukutana kwa mara ya kwanza mjini Cape Town Ijumaa baada ya matokeo ya uchaguzi kuonyesha kuwa hakuna chama kilichopata ushindi wa kutosha. Chama cha IFP kilipata viti 17 katika bunge la taifa lenye viti 400 ambapo wabunge wataitishwa kumteua spika na kumchagua rais wa nchi. Vyama vya kisiasa vimekuwa vikijitahidi kujenga muungano baada ya chama cha African National Congress cha Rais Cyril Ramaphosa kupoteza wingi wa kura kwa mara ya kwanza katika uchaguzi wa Mei 29.

Serikali ya Kenya imewasilisha kwenye bunge makadirio ya Bajeti ya mwaka 2024/25 ikitaka takriban shilingi trilioni 3.3 za mapato ya ushuru ili kufadhili bajeti ya pili ya shilingi trilioni 3.91 ya utawala wa Rais William Ruto, ambayo ndiyo kubwa zaidi nchini humo. Serikali imeweka mgao wa matumizi ya kawaida ya shilingi trilioni 1.5 na matumizi ya maendeleo kuwa shilingi bilioni 727.9 na kuitaja bajeti hiyo kama muhimu kukabiliana na deni la taifa na vile vile kulinda kuimarika kwa uchumi wake. Serikali ya Ruto inaitaja bajeti hii kuwa mwelekeo mwema wa uchumi katika nafasi ya ukuaji unaoongozwa na mauzo ya nje huku ikitenga rasilimali za ziada kuwezesha uzalishaji na ukamilishaji wa miradi inayoendelea ya miundombinu.

Bajeti ya serikali ya mwaka 2024/2025 iliyosomwa bungeni Alhamisi mjini Dodoma, serikali imeomba kuidhinishwa kwa jumla ya matumizi ya shilingi trillioni 49.35 ikiwa na ongezeko la asilimia 11 ikilinganishwa na bajeti ya 2023/2024. Wachumi wamesema kuwa licha ya serikali kuwa na kawaida ya kutengeneza bajeti ambazo ni nzuri na zinazotoa matumaini kwa wananchi, utekelezaji wa makadirio hayo umekuwa ukiwakatisha tamaa wananchi kutokana na bajeti hizo kutokutekelezwa kwa asilimia mia moja.

Rwanda ilisema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) lilidanganya lilipoiambia mahakama ya Uingereza wiki hii kwamba waomba hifadhi waliopelekwa katika nchi hiyo wanaweza kuhamishwa tena katika nchi ambazo wanakabiliwa na hatari ya kuteswa au kuuawa. Mawakili wanaoliwakilisha Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) walisema Jumatatu kuwa mfumo wa hifadhi ya Rwanda una mapungufu, kama sehemu ya changamoto kwa sera ya serikali ya Uingereza ya kuwafukuza wanaotafuta hifadhi huko.

Share