Matokeo mapya ya kura ya moani ya Newspoll yaliyo chapishwa katika gazeti la The Australian, imeonesha kuwa upinzani wa mseto una ongoza chama cha Labor kwa asilimia 51-49 katika kura ya upendeleo wa vyama viwili, wakati kura ya serikali ya shirikisho inasalia na uvutio wa asilimia 31, kulinganisha na asilimia 38 ya upinzani.
Wasafiri wameelezea hisia zao zaku fadhaika baada ya mamia ya huduma za treni za Sydney kufutwa asubuhi ya leo, huku wafanyikazi wa chama hicho wakichukua hatua za kiviwanda. Ijumaa asilimia 95.3 ya huduma zote zili cheleweshwa au zilifutwa. Shirika la Transport for New South Wales limesema hiyo ilikuwa kwa sababu idadi yama dereva wa treni 862 na walinzi, hawaku ripoti kazini kama kawaida. Tume ya Haki ya kazi ime tupilia mbali hoja ya serikali kuwa, hali isiyo tarajiwa ya idadi kubwa ya wafanyakazi walio dai wana umwa, naku amua hakuna muundo wa hatua iliyo ratibiwa.
Serikali ya New South Wales ina jiandaa kuwasilisha marekebisho ya mswada katika bunge la jimbo hilo hii leo Jumanne 18 Feb, kwa ajili ya kuwaadhibu watu wanaotoa matamshi ya kibaguzi ya rangi hadharani. Geuzi hilo lita ongeza kosa la uchochezi wa chuki la ubaguzi wa rangi katika sheria ya uhalifu, ambayo ikipitishwa ita kuwa na maana kwamba watu wanao thibitishwa kuwa walitoa kauli hizo katika umma, wanaweza tumikia kifungo cha miaka mbili gerezani pamoja nakupata faini ya zaidi ya $10,000.
Wakati huo huo kiongozi wa NSW Chris Minns amesema uhuru wa kauli yakisiasa chini ya mageuzi hayo na, kuwa kuna tofauti za kurejelea moja kwa moja maandishi yakidini wakati wa mafunzo yakidini.
Wendy Steendam atakuwa Kamishna Mkuu wa Jeshi la Polisi la Victoria, baada ya kujiuzulu kwa Shane Patton. Katika taarifa, Bw Patton amesema alifanya uamuzi huo kwa hiari yake kuondoka katika wadhifa huo, baada ya sehemu kubwa ya nguvu kazi yake kusema hawana imani na uongozi wake. Waziri wa Polisi wa Victoria, Anthony Carbines, amesema serikali ya jimbo hilo halita fichua maelezo kuhusu mazungumzo ambayo Bw Patton alifanya na mawaziri kabla ya kujiuzulu.
Rais William Ruto amekubali kushindwa kwa Kenya katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Muungano wa Afrika (AUC), akisema kwamba japo matokeo ya uchaguzi huo hayakumpendelea mgombeaji wa Kenya, “ningependa kushukuru kwa dhati uongozi mzima wa bara letu kuu.” Rais Ruto pia alimpongeza mwenyekiti mpya wa AUC, Mahmoud Youssouf na naibu wake Selma Haddadi.
Mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye ambaye alianza mgomo wa kula wiki iliyopita amekimbizwa hospitali jana jioni baada ya hali ya afya kuzorota. Hayo yameelezwa na mbunge mmoja mwenye mafangumano na Besigye na kuripotiwa pia na kituo kimoja cha televisheni nchini humo. Wanasheria wake wanasema "alitekwa nyara" nchi jirani ya Kenya na kusafirishwa kwa mabavu hadi nchini Uganda na kufunguliwa mashtaka kwenye mahakama ya kijeshi yanayojumuisha umiliki wa silaha kinyume cha sheria.
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imethibitisha kwamba jana Jumapili waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda waliukamata mji wa Bukavu ulio kwenye eneo tete mashariki mwa nchi hiyo. Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mawasiliano ya nchi imethibitisha kwa mara ya kwanza kuanguka kwa mji huo mkuu wa jimbo la Kivu Kusini na kusema kwamba serikali kuu mjini Kinshasa "inafanya kila inachowezesha kurejesha udhibiti" kwenye mji huo wa wakaazi wapatao milioni 1.3. Waasi wa M23 walitangaza tangu siku ya Ijumaa kuwa wameingia Bukavu na wameudhibiti mji huo bila upinzani wowote kutoka vikosi vya serikali.